Maofisa polisi 120 watimuliwa
Maofisa
wa Polisi wapatao 120 wa Jeshi la Polisi, waliokuwa wakihudhuria
mafunzo ya kupandishwa vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi
(MPA), wametimuliwa chuoni hapo.
Habari
za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya chuo hicho zamani
kikijulikana kama CCP, zimedai uamuzi wa kuwaondoa chuoni ulitangazwa
jana na mkuu wa chuo hicho, Matanga Mbushi.
Vyanzo
mbalimbali vililidokeza Mwananchi kuwa, waliotimuliwa chuoni hapo ni
maofisa ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali walioupata wakiwa
wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
Habari
hizo zilisema hadi jana saa 9:00 alasiri, maofisa hao walikuwa ofisi za
mkuu wa chuo hicho wakisubiri kupatiwa maelekezo ya namna ya kurejea
katika vituo vyao vya kazi mikoa mbalimbali.
“Wako
120 hivi walikuja hapa (MPA) kwa ajili ya kuchukua kozi za Koplo,
Sajenti, Meja na ‘Assistant Inspector’ (wakaguzi wasaidizi), lakini
ndiyo hivyo wametuambia tuondoke,” kilidokeza chanzo chetu.
Hata
hivyo, ofisa mmoja alilidokeza Mwananchi kwamba mkuu wa zamani Jeshi la
Polisi (IGP), Said Mwema, ambaye amestaafu, ndiye wa kulaumiwa kwa
kutoheshimu mapendekezo ya wataalamu.
“Tulimwambia
IGP Mwema kwamba ni vizuri kama maofisa wenye ulemavu kama baadhi ya
vigezo wanavyo basi wapewe vyeo huko huko mikoani, lakini wasiende
chuoni,” alidokeza na kuongeza;
“Tulipendekeza
yafunguliwe madarasa ya kanda wakishafanya mtihani wa kawaida wapewe
vyeo huko huko, lakini wakija chuoni ni lazima wahudhurie vipindi vyote
ambavyo vinafanya chuo kiitwe chuo.
“Chuo
chochote kile kina vigezo vyake na kwamba ili mtu apate cheo
alichokwenda kukisomea ni lazima ahudhurie asimilia 95 ya vipindi
ikiwamo kwata, medani za kivita na kuzuia vurugu,”alisema.
Chanzo
kingine kililidokeza Mwananchi kuwa maofisa hao waliripoti chuoni hapo
wiki mbili zilizopita na katika uchunguzi, walibainika wana ulemavu
ambao hawawezi kumudu mafunzo ya ukakamavu.
Mmoja
wa maofisa hao waliotimuliwa alilalamika kuwa kitendo hicho siyo cha
kiungwana kwa kuwa ulemavu huo waliupata wakiwa kazini wakilitumikia
Taifa na hawajashindwa kuingia darasani.
“Baadhi
yetu tumefanya kazi miaka 20 wengine 25. Wamekatika miguu. Wako trafiki
wamegongwa na polisi wengine wamepigwa risasi na majambazi wakapata
ulemavu si sawa kutunyima vyeo,” alidai.
Ofisa
huyo alisema pamoja na ulemavu huo, lakini wamekuwa wakipangiwa kazi na
kuzimudu kama kawaida isipokuwa zile za ukakamavu na kwamba hata wakati
wakipendekezwa, walikuwa wanajulikana matatizo yao.
Alipoulizwa
na Mwananchi jana, Mbushi alithibitisha kuwapo kwa uamuzi wa kuwaondoa
chuoni maofisa hao, lakini akasema wanasubiri maelekezo zaidi kutoka
makao makuu ya polisi.
“Bado
hatujawaondoa lakini ukweli ni kwamba kama mtu hawezi kumudu mafunzo
lazima aondolewe. Kama mtu hawezi kuingia kwenye paredi anakosa vigezo
vya chuo,” alisema na kuongeza;
“Tunawasiliana
na makao makuu ili tuone wataamua nini, lakini kwa kweli hawawezi
kumudu mafunzo ni wagonjwa wameumia, wengine miguu mibovu na mafunzo ni
ya kijeshi siyo darasani pekee,” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo wamependekezwa kupata vyeo kwa utaratibu wa kawaida kabisa ndani ya Jeshi la Polisi wanaingia darasani kama kawaida, lakini gwaride ambalo ni sehemu ya mafunzo hawawezi.”“Ni lazima tuchukue kila aina ya tahadhari unaweza kulazimisha halafu mtu akafa kwa sababu mafunzo hasa ya ujasiri ni magumu, lakini kumbe mtu amekuja ni mgonjwa,” alisisitiza Mbushi na kuongeza;