Thursday, 12 February 2015

Masaju: ‘ Ratiba ya kura ya maoni haitobadilishwa ’

Masaju: ‘ Ratiba ya kura ya maoni haitobadilishwa ’


Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa ratiba ya kura ya maoni iko pale pale na kusisitiza kuwa ni lazima kura ya maoni ifanyike Aprili 30 mwaka huu.
Akizungumza  muda mfupi baada ya kukutana na wahariri wa vyombo vya habari  jana, Masaju amewataka wananchi kuondoa hofu juu ya uwezekano wa kufanyika kwa kura ya maoni kwa madai muda uliopo hautoshi kwa ajili ya maamuzi kuhusu Katiba inayopendekezwa kufanyika hapo Aprili 30.
Ameongeza kuwa mchakato wa Katiba mpya unaendelea vizuri na kwamba muda uliopo unatosha kwa ajili ya zoezi la kampeni pamoja na kupiga kura ya maoni.
Kwa upande mwingine  amesisitiza  kuwa zoezi la elimu kwa umma, kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kampeni vinaweza kufanyika kwa pamoja.

clouds stream