Machungu’ ya mgao wa umeme nchini kuanza leo
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetangaza kuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa kuanzia lleo. Hatua hiyo inatokana na kuzimwa mitambo yote ya umeme katika kituo kikubwa cha kuzalisha umeme cha Ubungo, Dar es Salaam kwa nia ya kuingiza gesi asilia katika mitambo huo.
Mgao huo unadaiwa kuwa utadumu kwa wiki nzima ukihusisha umeme kukatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo hicho kikubwa.
Alisema kwa saa za mchana na usiku ndani ya wiki hii itakuwa mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa itakosa umeme.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema kwa sasa mitambo ya Kinyerezi imejaa gesi na wameishaingiza gesi yenye mgandamizo wa tatu na inatakiwa kufika mgandamizo 50 hadi 51 ili kuzalisha umeme.
Amesisitza kuwa kuwa uzalishaji huo, Serikali itaokoa dola bilioni moja zilizokuwa zikitumika kwa uzalishaji umeme wa mafuta.