Royal Penthouse Suite, Hotel President Wilson, Geneva (TSH mil
104 kwa usiku)
kwa sababu za
kiulinzi zaidi pamoja na usalama hakuna hoteli duniani inayosifika kama President
Wilson hotel ambapo katika muonekano wa chumba utaona ziwa Geneva na pia ziwa
Mont Blanc. Vioo vya chumba hiki vinauwezo wa kuzuia risasi na ina lifti yake
binafsi kwa anetumia chumba hicho. Chumba hiki pia kina eneo la mazoezi, chumba
cha kikao na pia eneo la muziki.
The Presidential Suite, The Raj Palace Hotel, Jaipur, India (TSH MIL 72 Kwa usiku)
Hoteli ya Raj ina
historia ya kua chumba kikubwa zaidi kuliko vyote vyenye hadi ya kiraisi kwa
bara Asia. Ukubwa wake ni kama mita mraba 1500. Chumba hiki kimepambwa kwa
dhahabu, pembe za ndovu na vioo vilivyowekwa kwa ustadi wa aina yake. Chumba
hiki kina bwawa la kuogelea, makumbusho binafsi na uzuri wake unaeza kukufanya
usitamani kuondoka.
Ty Warner Penthouse Suite, Four Seasons Hotel, New York (TSH MIL
66.93 kwa usiku)
Chumba hiki kina mita za mraba 400 ambacho
kiko juu kabisa na kinakupa muonekano wote wa Manhattan New York. Chumba hiki kimepambwa na platinum pamoja na
dhahabu na kina garden ya ndani kwa ndani. Ukiwa kwenye chumba hiki utapata
waiter wako binafsi, mkufunzi wa mazoezi au mesaji wako binafsi pamoja na
dereva wako binafsi
Ritz-Carlton Suite, Ritz-Carlton, Moscow (TSH MIL 28.8 kwa
usiku)
Dari la hoteli hi kwa kipekee zaidi limefanana
nan a tiles safi zenye taa nyingi za rangi mbali mbali kuweka nakshi. Chumba
hiki kina mita za mraba 232 na kna eneo la chakula, ofisi, library na kwa
sababu ya baridi mjini Moscow sakafu yake ina heater.