Friday, 24 June 2016

Uingereza Yapiga Kura Kujitoa EU


Tarehe June 24, 2016DE2BC789-63F0-40ED-A5F3-24462FCFBB2D_w987_r1_s
Kiongozi wa kampeni ya kujitoa Nigel Farage akishangilia baada ya matokeo kutangazwa
Yakiwa yamebaki majimbo matano Kati ya 382 kutangazwa, Uingereza wamepiga Kura kujitoa katika Umoja wa Ulaya baada ya miaka 48.
Shirika la habari la ITV na Sky news huko Uingereza yote kwa pamoja yametangaza kambi ya kuondoka imeshinda ikiwa na kura zaidi ya milioni moja na laki moja, sawa na asilimia 52 ya kura zote.
Tume ya uchaguzi ya Uingereza imeeleza kuwa watu wengi wamejitokeza kupiga kura hiyo ambayo inagusa masuala ya uhamiaji uhuru , usalama na siku zijazo za uchumi wa Uingereza.
“Maafisa wa upigaji kura wamethibitisha kuwa jumla ya kura 33,568,184 zitajumuishwa katika kura ya maoni. Kwa mujibu wa watu waliojitokeza kupiga kura waliothibitishwa kuwa 46,500,001, waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 72.2,” tume hiyo ilisema katika taarifa yake.
Kiongozi wa kampeni ya kujitoa Nigel Farage amesema Juni 23 itakumbukwa kihistoria kama siku ya uhuru na kumtaka waziri mkuu David Cameron kujiuzulu.

clouds stream