Lowassa alipua upya sakata la Richmond, alia na Mwakyembe
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ameibuka kwa mara ya kwanza na kuzungumzia sakata la Richmond lililopelekea kujiuzulu cheo cha Uwaziri mkuu febriari 7 mwaka 2008.
Akizungumza na Wahariri leo nyumbani kwake mkoani Dodoma Edward Lowassa amesema kwamba hausiki kabisa na sakata ka Richmond na ndio sababu hata kamati a Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Nazir Kalamagi, Peter Selukamba, Diana Chilolo, Hussein Bashe ikiwa ni baadhi ya walio athirika kutokana na sakata la Richmond. Katika mkutano huo pia amemtangaza Elizabeth Msoki kuwa mkurugenzi wa mahusiano na Mawasiliano katika timu yake ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Ameongeza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio lilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na Spika wa Bunge wa wakati huo ambaye alikuwa ni Samweli Sitta. Hicho sio kikwaz kwake katika safari yake ya kuingia ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua huku akiahidi kuchukua muda mrefu zaidi kulizungumzia sakata hili hususani mwishoni mwa wiki hii mkoani Arusha.
Lowassa alijiuzulu februari 7 mwaka 2008 kutokana na madai ya kuhusika ktika kashfa ya kuibeba kampuni ya Richmond Development (LLC) ya nchini Marekani katika mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya umeme wa dharura hapa nchini.
Akizungumzia malengo yake Lowassa amesema serikali ya Jakaya ilikosea kuanza kilimo na kuweka kando elimu huku akisisitiza sera yake itakuwa ni elimu kwanza.
Kwa upande wa Pesa za kampeni amesema anapata kutokana na michango ya rafiki zake na ataendelea na kupata michango hiyo.
Alipoulizwa kuhusu mpango wa kuhama Chama chake endapo atatatoswa na kamati kuu (CCM) amesema asiyempenda ndani ya chama hicho atahama yeye kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi ya kuwania Urais huku akisisitiza kuwa hatalipa kisasi kwa jambo lolote lililomtokea katika safari yake ya kisiasa ikiwemo sakata la Richmond.
Hata hivyo amesema Arusha itwaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ata aanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuinua nchi kuichumi katika miaka kumi ijayo.