Thursday 28 July 2016

Miaka Miwili Jela Kwa Kukashifu Au Kutumia Vibaya Vielelezo Vya Taifa


Tarehe July 28, 20161000px-Coat_of_arms_of_Tanzania Mpiga Chapa wa Serikali amesema ni kosa kisheria kutoa lugha chafu ya kukashifu au kuandika maneno yenye lengo la kudhihaki bendera au nembo yoyote ya Taifa kwani kosa hilo linaweza kupelekea mtuhumiwa kufungwa kifungo gerezani kisichozidi miaka miwili.
Akiongea Jijini Dar es Salaam, Mpiga Chapa wa Serikali, Kassian Chibogoyo amesema wananchi wote wanapaswa kuheshimu vielelezo vya Taifa ikiwemo wimbo wa Taifa na nembo ya Taifa.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ya mwaka 1971 na Sheria ya Bendera ya Taifa ya mwaka 1962 na Sheria ya Ngao ya Taifa pamoja na Sheria ya Alama za Taifa, zinamkataza mtu yeyote kutumia bendera ya Taifa, ngao ya Taifa au nembo ya Taifa kinyume na ilivyokusudiwa,” amesema.
Kwa mujibu wa Chibogoyo, sheria hizo zinamkataza mtu yeyote kutumia bendera, nembo ya Taifa au kitu chochote kinachofanana na bendera au ngao ya Taifa kama alama ya biashara, shughuli za kitaaluma au kwenye maandiko yoyote yanayokusudia mauzo.
Hivi karibuni imekuwa ni jambo la kawaida kukuta wananchi wakiwa wameweka bendera za Taifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika vyombo vya usafiri kama magari binafsi, daladala na hata bodaboda ambapo baadhi ya vyombo hivyo ni vya biashara

clouds stream