Monday, 28 July 2014

JINSI MOURYNHO ANAVYOMUONA DROGBA

Mourinho : Drogba ni mChelsea damu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.
Mourinho alidhibitisha kuwa The Blues inatafakari kurejea kwake Uingereza na kuwa anatumai uhamisho huo utatekelezwa bila hisia kali .
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
Drogba akiwa Galatasaray.
Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich .

Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.

ARSENAL KUMSAJILI CHAMBERS.

Arsenal yamsajili Chambers
Kilabu ya Uingereza ya Arsenal imemsajili mlinzi wa kilabu ya Southampton Calum Chambers kwa takriban paundi millioni 16.
Mchezaji huyo wa timu ya Uingereza isiozidi umri wa miaka 19 alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya ijumaa.
Chambers mwenye umri wa miaka 19 ameshiriki mara 25 katika timu ya soka ya taifa la Uingereza na kwamba Arsenal inamuona kama suluhu wa safu ya ulinzi wa kulia na katikati .

Arsenal pia inamsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliichezea timu ya Ufaransa katika kombe la dunia.

LIVERPOOL YAMSAJILI ORIGI

Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji 
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Divorc Origi hatimaye amejiunga na timu ya Liverpool.

Baba yake Origi, Mike Okoth, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu taifa ya Kenya Harambee Stars amethibitsha mwanawe Divorc amesaini mkataba na Liverpool ambao walifurahishwa na mchezo wake mzuri alipoiwakilisha Ubelgiji kwenye kombe la dunia.

Sunday, 20 July 2014

PLOTS FOR SALE


  • ENEO LA EKA 8 LINAUZWA LIPO SALASALA KWA SH MILLION 500
  • MASHAMBA NA PLOT ZINAUZWA KIBAHA TAMCO KWA EKA 1 SH MIL 10. PIA ZINGINE ZIPO MKURANGA, MBEZI LOIUS, GOBA NA BUYU.
  • Eneo linataka mwekezaji wa kujenga apartments. Lipo jirani na CSAURP ukubwa wa eka moja
  • eneo linauzwa SQM 1500 na ni eneo la kibiashara. lipo mwnge jirani na Tamal hotel kwa bilioni 1.

Wednesday, 16 July 2014

ISRAEL YAZIDI KUUA.


Israel imezidisha mashambulio baada ya mapendekezo ya kusitisha mapigano kutibuka
Jeshi la Israel limesema kuwa limetoa onyo tena kwa wakaazi wa mashariki na kaskazni mwa Gaza kuondoka majumbani mwao kwani wanaendeleza mashambulizi zaidi.
Onyo hili linajiri wakati majaribio ya kusitisha mapigano katika eneo hilo la Palestina yakionekana kutibuka.

Habari za punde zasema mashambulizi hayo ya Israeli yamelenga na kupiga nyumba za viongozi wa juu wa Hamas Mahmoud al-Zahar, na pia ile ya waziri wa zamani wa usalama wa ndani ya nchi Fathi Hamad.Maafisa wa jeshi wamesema kuwa maeneo mengi yanayotumiwa kurusha maroketi kutoka Gaza yamelipuliwa huku kundi la Hamas likiendeleza mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel.
Mwanamme mmoja mu-Israeli ameripotiwa kufariki alipogongwa na magruneti ya Hamas alipokuwa amekwenda kuwapelekea chakula wanajeshi wa Israel walioko karibu na mpaka wa Gaza.
vifo vingi na majeruhi yametokea miongoni mwa raia wa wapestina
Zaidi wa Palestiniana 200 wamefariki katika mashambulio haya ya sasa, wengi wamejeruhiwa, huku majumba na miundombinu ya Gaza ikiwa imeharibiwa sana.
Israel inadai imelazimika kuongeza mashambulio kwani Hamas wamekataa majadiliano ya kidiplomasia.
Hata hivyo msemaji wa Hamas, Osama Hamdan, ameiambia BBC kuwa hawaiamini Israel na hivyo hawawezi kuzungumzia mpango wa Amani wanaousikia tu kupitia vyombo vya habari kwani mpango kama huo hauwezi kamwe kuwasaidia wa- Palestina.
Inasemekana mapendekezo hayo sasa yamewasilishwa rasmi na Hamas wamesema wako tayari kuyajadili.
Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu huko Gaza yanasema mashambulizi hayo ya Israeli yameharibu hata miundo mbinu ya maji na upungufu mkubwa maji unajiri.
Shirika la umoja wa mataifa la misaada linasema mfumo wa maji machafu haufanyi kazi kamwe na asilimia 90 ya maji yaliyoko si safi kwa matumizi ya binadamu.

Monday, 14 July 2014

HOUSE FOR SALE TABATA KWA BIBI

LOCATION: TABATA KWA BIBI

FEATURES:  4 BEDROOMS 2 BEING MASTER BEDROOMS, KITCHEN, DINNING, STORAGE ROOM

AREA: SQM 900

PRICE: 160 MIL

CONTACT: +255 652 314 181

EMAIL: nijuzetz@gmail.com or rocklandrealestate1@gmail.com.




Tuesday, 8 July 2014

MAPACHA TIME FOR THE MONEY.

OFFICES TO LET

OFFICES TO LET located along Ali Hassan Mwinyi road and Makumbusho, SPACES CONTAIN.

  • RESTAURANT SPACE
  • SPACE FOR OFFICES
  • BANK ATM SPACES
  • BANK OFFICE SPACES
PRICES AND OTHER DETAILS MAY BE DISCLOSED VIA CONTACTS WI THE FOLLOWING LINK

NO. +255652314181 OR EMAIL: nijuzetz@gmail.com








YARD FOR SALE  LOCATED NEAR THE NEW MAKUMBUSHO BUS STAND. SQM 1089 PRICED AT TSH 1.5 BILLION NEGOTIABLE.

HOUSE FOR SALE AT TABATA BIMA

LOCATION: TABATA BIMA

FEATURES: 3 BEDROOM, KITCHEN, DINNING AND SITTING ROOMS, HAS A BACK HOUSE WITH TWO BEDROOMS, STORE SITTING ROOM A PRIVATE WASHROOM.

AREA: SQM 720

PRICE: TSH 250 MIL NEGOTIABLE.

CONTACTS: +255652314181 

EMAIL: rocklandrealestate1@gmail.com / nijuzetz@gmail.com




Monday, 7 July 2014

WEBB HUENDA AKACHEZESHA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2014


Refarii Howard Webb
Referii muingereza anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa waamuzi 15 walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Webb mwenye umri wa miaka 42 ni miongoni mwa wale watakaotathminiwa kwa uwezo wao wa kuamua mechi zenye umuhimu mkubwa ikiwemo fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Webb pamoja na wasaidizi wake Mike Mullarkey na Darren Cann wamekwisha amua mechi mbili za kombe la dunia huko Brazil.
Webb ni kati ya waamuzi 15 waliosalia Brazil
Mpiga kipenga huyo alikuwa muamuzi katika mechi kati ya Colombia na Ivory Coast na pia mechi baina ya wenyeji Brazil na Chile.
Webb alijiimarisha wasifu wake mwaka wa 2010 alipoamua mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya uhispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini .
Webb ndiye aliyeamua fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010
Webb hata hivyo alilaumiwa kwa kukosa kumwadhibu mchezaji Nigel de Jongfor .
Na baada ya kutizama kanda za video Webb alikiiri kuwa alistahili kumwonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kadi nyekundu .
Refarii mmoja pekee kutoka Brazili, Sandro Ricci ndiye aliyesalia kuamua mechi zilizosalia za nusu fainali fainali na mechi ya kuamua mshindi wa tatu.
Mbali na Brazili Argentina, Ujerumani na Uholanzi ndiyo mataifa yaliyosalia katika kipute hicho.
Refarii Marco Rodriguez ndiye aliyakosa tukio la Suarez kumng'ata Chiellini
Refarii kutoka Mexico Marco Rodriguez ndiye atakayeamua mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya Ujerumani na wenyeji Brazil.
Mechi hiyo itachezwa Jumanne .
Rodriguez ndiye refarii ambaye alikosa kumuona mshambulizi wa Uruguay Luiz Suarez akimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.

clouds stream