Iwapo kutakuwa na taarifa zozote za kuibuka kwa
ugonjwa huo, tayari kambi maalumu za kuwatambua wagonjwa wa ebola
zimeshaanzishwa katika× Kikuu cha Tiba na× Sayansi cha Muhimbili ambako watafanyiwa uchunguzi na watakaobainika watapelekwa katika kituo maalumu cha kuwahifadhi kilichoko katika× Hospitali ya Temeke.
Dar es Salaam. Tanzania ni
miongoni mwa nchi 15 zilizoko katika hatari ya kupata mlipuko wa ugonjwa
wa ebola kwa mujibu wa maelezo ya wanasayansi.
Wanasayansi hao wa× Kikuu cha Oxford nchini× Uingereza pia wameainisha kuwa zaidi ya watu milioni 22 barani× Afrika wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Hadhari hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na× Serikali
ikiwahakikishia wananchi wake kwamba iko katika jitihada ya kuandaa
mazingira ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini.
Wakati wanasayansi hao wakisema hayo, wiki
iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alikagua maandalizi ya kituo cha kupokea
wagonjwa wa ebola eneo la Temeke na mitambo iliyowekwa Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) endapo watapatikana wasafiri wenye
dalili za maradhi hayo.
Vilevile kuona jinsi wahusika walivyopewa mafunzo maalumu ya kuwahudumia wagonjwa hao.
Tayari mitambo hiyo imeshafungwa katika Viwanja
vikubwa vya ndege vya Kilimanjaro (KIA), JNIA, Uwanja wa Ndege wa
Zanzibar na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Citizen toleo
la jana, mamlaka zilizoko chini ya Wizara ya Afya zimeendelea
kukabiliana na hofu ya kuibuka kwa ugonjwa huo hatari uliozikumba nchi
nyingi za Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.
Iwapo kutakuwa na taarifa zozote za kuibuka kwa
ugonjwa huo, tayari kambi maalumu za kuwatambua wagonjwa wa ebola
zimeshaanzishwa katika Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi cha Muhimbili
ambako watafanyiwa uchunguzi na watakaobainika watapelekwa katika kituo
maalumu cha kuwahifadhi kilichoko katika Hospitali ya Temeke.
Kengele ya hatari
Ugunduzi mpya uliofanywa katika eneo ambalo ebola
imeonyesha athari kubwa Afrika Magharibi umezidi kutoa ishara ya hatari
kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo mlipuko haukuwahi
kuripotiwa.
Serikali za nchi hizo zimehadharushwa kuwa
zinatakiwa zijipange kwa kujua njia na namna ya kukabiliana na tishio
hilo badala ya kuelekeza nguvu katika kuwabaini waathiriwa kupitia
viwanja vya ndege na bandari pekee.