Saturday, 21 October 2017

ZITTO AIBUA MAPYA BAADA YA ACACIA KUDAI HAINA HELA YA KULIPA






Wakati Watanzania wakiwa katika hali ya sintofahamu baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Acacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa juzi na Kampuni ya Barrick Gold Mining, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACTWazalendo),Zitto Kabwe ameibuka tena na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Mhe. Kabwe amesema kuwa alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwaKampuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (akiiita kishika uchumba) ambapo hata mwaka 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi waliahidi hivyo.

Amesema kwamba tangu juzi alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba “Tumefanikiwa” kwani haikuwa ikizungumza nakampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya makampuni, mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

“Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadikama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Acacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo,” amesema Zitto.

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa Dola milioni 300 (sawa na zaidi ya bilioni 660) kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro uliokuwepo awali.

clouds stream