In Summary
Moja ya mashauri yaliyokuwa yakijadiliwa hapo juzi ni kesi iliyofunguliwa na× Yanga kupinga uamuzi wa mshambuliaji wao× Okwi kujiunga na Simba wakati bado akiwa na mkataba na klabu hiyo.
Kamati hiyo iliketi kuanzia muda wa saa 9.30
alasiri hadi saa 12:15 jioni (dakika 165) ambapo pande mbili yaani
walalamikaji (Yanga) wakiongozwa na× Mkuu wa klabu hiyo× Njovu na mwanasheria wao× Mapande na mlalamikiwa (Okwi) akiwa na mwanasheria× Ndumbaro, ambaye alimwakilisha mwanasheria wa Okwi, Edgar Aggaba waliondoka ukumbini hapo.
Hali ilivyokuwa
Kamati ilitoa fursa kwa Yanga kuwasilisha
vielelezo vyote juu ya hoja zao ambapo Mapande na Njovu walifanya hivyo
kabla ya baadae Okwi na Ndumbaro kuambiwa wapeleke utetezi wao.
Kamati ilichukua muda wa saa mbili kusikiliza
pande hizo mbili na kupeana mapumziko mafupi kabla ya kurejea tena
kumalizia mashauri hayo. Hata hivyo utulivu uliendelea kutawala hotelini
hapo huku wajumbe wakiingia na kutoka katika chumba cha majadiliano.
Pande zote mbili zilionekana kuwa na matumaini ya
kushinda kesi hiyo lakini baadaye upande wa Okwi na Ndumbaro ulionekana
kuwa na mashaka kuwa endapo Kamati hiyo itaamua kutoa uamuzi wake kwa
kupiga kura basi ‘ingekula kwao’.
Wasiwasi huo ulitokana na dhana ya kwamba kamati
hiyo ina wajumbe wengi ambao ni wanachama wa Yanga akiwemo mwanasheria
Iman Madega aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga na Abdul Sauko aliyekuwa
Katibu Mkuu wa klabu hiyo huku upande wa Simba ukidaiwa kuwa na wajumbe
wawili tu mmoja wapo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo,
Zacharia Hans Poppe.
Ukumbi wabadilishwa
Awali hukumu hiyo ilipangwa kufanyika katika ofisi
za TFF kama ambavyo wajumbe walitangaziwa awali lakini kwa hofu ya
kutaka utulivu hasa kwa lengo la kutaka kuwakimbia makomandoo wa Simba
na Yanga ukumbi huo ulibadilishwa haraka na kupelekwa katika hoteli ya
Colosseum ambako ndiyo kila kitu kilimalizika huko.
TFF baada ya kufika Colosseum walikosa ukumbi wa
kufanyia mkutano baada ya hoteli hiyo kujaa hawakuwa na mbadala mwingine
zaidi ya kutafuta chumba na kupatiwa chumba namba 201 ghorofa ya pili
ambako ndipo kila kitu kilifanyika hapo.
Hoja ya Yanga yadunda