RAIS WA SUDAN KUSINI AANGUKA UWANJA WA NDEGE

Katika hali isiyotegemewa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameanguka chini muda mfupi baada ya kuwasili kwenye mji mkuu wa Sudan,Khartoum kukutana na Rais wa Sudan Omar al Bashir,baada ya tukio hilo maafisa wa Ulinzi wa Rais Salva Kiir waliamuru kwa nguvu mwandishi aliyepiga picha ya tukio hilo azifute mara moja ili kuondoa ushahidi wa tukio hilo.Watu walifuatilia tukio hilo wanasema chanzo cha Rais Salva Kiir kuanguka ni kuchoka,pia baada ya madaktari kufanya uchunguzin aliondoka na gari uwanja wa ndege