WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JESHI LA POLISI 2014
,
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa majina ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2013 na cha sita mwaka 2014. Angalia hapa umechaguliwa kwenda chuo kipi cha mafunzo ya Polisi.
Maelekezo Muhimu.
- Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
- Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
- Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
- Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.
- Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
- Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
- Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
- Chandarua chenye upana futi tatu
- Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
- Pasi ya Mkaa
- Ndoo moja
- Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
- Pesa kidogo ya kujikimu.
- Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.