RAIS WA UKRAINE APINGA UCHAGUZI
Rais Petro Poroshenko wa Ukraine amesema kuwa hatambui uchaguzi unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo na kwamba kwa hatua hiyo wanarudisha nyuma jitihada za kuleta amani nchini humo.
Katika hotuba yake iliyoonyeshwa kwenye Runinga pia Poroshenko amesema kuwa serikali yake haitatambua upigaji kura huo katika majimbo ya Donetsk and Luhansk kutokana na kuwepo machafuko hivyo kukosekana amani.
Hata hivyo amesema kuwa hali ya machafuko katika mashariki mwa taifa hilo kumesababisha kuvunjika kwa hali ya amani na kuleta vurugu.
Katika hatua nyingine, Poroshenko amesema kuwa anatarajia kupendekeza sheria itakayopiga marufuku waasi katika eneo ambalo limepitishwa na kuwa eneo lenye harakati za kutaka kuleta amani.