KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI
Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Aidha.Bw Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Katika tukio la mauaji ya watu 28 ambapo wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri ambao hawangeweza kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani ya Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.