ENTENTE SATIF MABINGWA WA AFRIKA 2014/15

Viongozi na wachezaji wa Entente Satif wakishangilia ubingwa wao baada ya kuuchukua mbele ya AS VitaClub.
Raundi ya pili ya fainali katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida ilikamilika kwa sare ya 1-1,siku sita baada ya sare ya 2-2 katika mechi ya kwanza iliochezwa mjini Kinshasa.
Setif ilianza kuona lango na wapinzani wao dakika nne katika kipindi cha pili kupitia Sofaine Younes ambaye alifunga bao kupitia pasi ya El Hadi Belameiri.
Lakini wageni hao walisawazisha dakika tano baadaye kupitia Lema mabidi aliyepiga mkwaju kutoka nje ya eneo la kupigia penalti ili kuimarisha matumaini ya timu yake.
Mabidi pia alikuwa ameifungia kilabu hiyo mabao yake mawili katika raundi ya kwanza ya mchuano huo wikendi iliopita.
Bao hilo lilisababisha mechi hiyo kuwa ngumu ambapo Vita ilionyesha mchezo mzuri ikilinganishwa na wapinzani wao Setif waliojaribu kutumia mbinu chafu za kupoteza mda huku mashabiki wa kilabu hiyo wakitaka mchezo huo kukamilishwa kuanzia dakika ya 75.