Thursday 2 November 2017

Mahakama Yasitisha Uchaguzi Liberia






Mahakama ya juu zaidi nchini Liberia imeamrisha maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kusitishwa kufuatia madai ya udanganyifu kutoka kwa mgombea aliyeondolewa kutoka kinyanganyiro hicho.

Mcheza soka wa zamani George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai wanatarajiwa kukutana katika duru hiyo ya pili ya  Uchaguzi Novemba 7, mwaka huu.

Lakini mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alishika nafasi ya tatu amepinga matokeo hayo ya awali akituhumu kuwa kulikuwa na udanganyifu.

Uchaguzi wa mwezi uliopita ndio wa kwanza huru kufanyika tangu kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003
nchini humo.

Mahakama imeamrisha chama cha Liberty na tume ya uchaguzi nchini humo kupeleka kesi zao ifikapo Alhamisi.

Lakini msemaji wa Tume ya Uchaguzi, Henry Flomo amenukuliwa akisema kuwa hajajulishwa rasmi kuhusu amri hiyo ya
mahakama.

Waangalizi wa kimataifa wakiwemo wale kutoka muungano wa Ulaya hawajaelezea hitilafu yoyote wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi.

clouds stream