Wednesday, 1 November 2017

UEFA: Man U yaichapa Benfica 2-0


Kwa mara ya mwisho Daley Blind kufunga goli ilikuwa Desemba 2016Kwa mara ya mwisho Daley Blind kufunga goli ilikuwa Desemba 2016

Manchester United ikiwa nyumbani katika dimba la Old Trafford imefanikiwa kuichapa Benfica 2-0 na kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne inaweza kuingia katika hatua ya mtoano.

United ambayo imeingia katika mashindano hayo kwa kuchukua kikombe cha ligi ya Europa msimu uliopita wameshinda michezo yote minne waliocheza na hivyo wanahitaji alama moja pekee katika michezo miwili iliyosalia ili kuweza kufuzu moja kwa moja.

Anthony Martial, ambaye alikuwa tishio katika mchezo huo, alikosa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa katika eneo la hatari na Douglas na mkwaju wake kuchezwa na mlinda mlango wa Benfica Mile Svilar ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.

Licha ya kushindwa kufunga mkwaju wa penalti, Antony Martial alionyesha kiwango boraLicha ya kushindwa kufunga mkwaju wa penalti, Antony Martial alionyesha kiwango bora

Svilar aliokoa pia mikwaju miwili mikali ya Mbelgiji mwenzake Romelu Lukaku kabla ya kujifunga goli la kwanza baada ya mkwaju mkali wa Nemanja Matic kumgonga mgongoni.

Marcos Rashford aliyeingia kipindi cha pili aliongeza mashambulizi zaidi kwa upande wa Manchester United na kusababisha penalti ambayo ilifungwa vyema na Daley Blind.

Benfica ilionyesha kiwango kizuri lakini mlinda mlango wa Man U David de Gea aliokoa mikwaju yao yote.

Kwa matokeo hayo Man U inaongoza ikiwa na alama 12, huku Benfica ikiburuta mkia na alama 0.

Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York

Marekani

Shambulizi nchini Marekani baisikeli na miili ya watu ilitapakaa ardhini



Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo.

Bill amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo.

Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyetekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.

Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.

Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii.
Marekani

Gari lililosababisha tukio hilo

Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Lower Manhattan.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baisikeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Lower Manhattan ya chini ,kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.

Raila Odinga: ''Hatutambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta''

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila OdingaKiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Nasa Raila Odinga ameapa kuendelea kufanya maandamano dhidi ya uchaguzi wa Uhuru Kenyatta akisisitiza kuwa upinzani haumtambui.

Odinga anasema kuwa Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya baadhi ya makamishna katika tume hiyo.

Odinga ambaye alikuwa akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee.

Anasema kwamba iwapo uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote.

Mr Odinga pia amesema kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na demokrasia ilipatikana.

Amesema kuwa iwapo uchaguzi wa Uhuru utaruhusiwa kuna uwezekano kwamba ataingilia katiba na kuongeza muhula wa kuongoza.

''Tutaendelea kufanya maandamno kila mara'', alisema Raila Odinga.

Rais Uhuru Kenyatta baada ya kutangazwa mshindiRais Uhuru Kenyatta baada ya kutangazwa mshindi

Bwana Odinga alisusia uchaguzi wa marudio wa urais wiki iliopita kwa sababu anasema kuwa hakuna mabadiliko yaliofanyiwa tume ya uchaguzi ya IEBC baada ya mahakama ya juu kupata makosa na ukiukaji mkubwa wa katiba.

Watu waliojitokeza kupiga kura ni chini ya asilimia 39.

Ametangaza kuwa atazindua bunge la wananchi ambalo litashirikisha jopo litakalochunguza kufeli kwa tume za uchaguzi.

clouds stream