Monday, 22 June 2015

Kombe la FIFA kwa wanawake,Cameroon yatupwa nje

Kombe la FIFA kwa wanawake,Cameroon yatupwa nje

Tarehe June 22, 2015
Mechi  kombe la FIFA la dunia kwa  wanawake zapamba moto.
Mechi kombe la FIFA la dunia kwa wanawake zapamba moto.
Mechi  kombe la FIFA la dunia kwa  wanawake zinazoendelea nchini Canada ambapo michezo ya hatua ya mtoano ya 16 bora inafanyika kwa sasa huku mwakilishi pekee kutoka Barani Afrika Cameroon  akitolewa.
Aidha, Katika michezo iliyochezwa mwishoni mwa juma wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia katika fainali hizo Cameroon wamesukumizwa nje baada ya kula mweleka wa goli moja kwa bila dhidi ya China, huku Australia, Ufaransa na wenyeji wa Canada wakiungana na China kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.
Bao pekee lililofungwa dakika ya 80 ya mchezo na Kyah simon limetosha kuwapa ushindi wa goli moja kwa BILA kinadada wa AutsraliA dhidi ya brazil na kuwavusha katika hatua ya robo fainali.
Katika matokeo mengine nyota wa ufaransa, marie laure delie alifunga magoli Mawili huku bao lingine likifungwa na elo die thomis na kuwapa ufaransa ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya korea kusini na hivyo kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
Wenyeji Canada nao wamepata ushindi wa goli Moja kwa bila dhidi ya Switzeland na kufuzu hatua ya robo fainali.
Leo inachezwa michezo mingine miwili kuwania kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali ambapo bingwa wa zamani wa dunia  Norway wakiwa na ukame wa miaka 20 wa taji hilo wanachuana na England.

Sheikh Mkuu wa Tanzania apatikana

Sheikh Mkuu wa Tanzania apatikana

Tarehe June 22, 2015
Sheikh Aboubakar Zuberi.
Sheikh Aboubakar Zuberi.
Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) asubuhi ya leo lamteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti mpya wa muda.
Hatua ya uteuzi huo inafuatia kifo cha aliyekuwa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Issa Shaaban Bin Simba aliyefariki kutokana na  shinikizo la damu na kisukari katika Hospitali ya TMJ na kuzikwa mkoani Shinyanga wiki iliyopita.
Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.

Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani

Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani

Tarehe June 22, 2015
Rais Omar el Bashir akiwa nchini Afrika kusini kwa mkutano wa viongozi wa Afrika.
Rais Omar el Bashir akiwa nchini Afrika kusini kwa mkutano wa viongozi wa Afrika.
Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Katika tukio hilo nusura rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe. Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
Kwa mujibu wa  gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka katiba.
Katika taarifa yake,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini humo.
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.

clouds stream