Saturday, 9 April 2016

Maalim Seif Kutoa Msimamo Wake Urais Wa Dr. Shein Z’bar

Maalim Seif Kutoa Msimamo Wake Urais Wa Dr. Shein Z’bar

Tarehe April 9, 2016Maalim Seif katika moja ya mikutano yake ya kisiasa.
Maalim Seif katika moja ya mikutano yake ya kisiasa.
Maalim Seif katika moja ya mikutano yake ya kisiasa.
Hatimaye Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20,2016
Inadaiwa kuwa kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza  tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.
Uamuzi huo unafuatia ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.
Aidha, CUF  ilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana kufuatia  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani kwa madai  ya kuwepo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Ridhiwani Kikwete Aibuka, Aikana ‘Kweupe’ Kampuni Ya Lugumi

Ridhiwani Kikwete Aibuka, Aikana ‘Kweupe’ Kampuni Ya Lugumi

Tarehe April 9, 20161
1
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.
Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo, Said Lugumi.
“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani
Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi baada ya kampuni hiyo kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 18 vya polisi badala ya 108 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba.
Kwa mujibu wa PAC, mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote lakini imeshindwa kumaliza kazi iliyopewa.

Mrema Amuangukia Magufuli Ampe Kazi

Mrema Amuangukia Magufuli Ampe Kazi

Tarehe April 9, 2016Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema.
Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amuangukia Rais Dkt. John Magufuli ampe kazi ili amsaidie kutumbua majipu.
Mrema amemuomba Rais kazi wakati akiongea na Waandishi wa Habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa wakati wa Kampeni Rais Magufuli alimuahidi kumpa kazi endapo angeshinda urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini cha kushangaza hadi sasa hajampa.
Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.
Mwanasiasa huyo pia  alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

clouds stream