Saturday, 19 November 2016

Mji wa Aleppo wakumbwa na mashambulizi makali

Vikosi vya serikali vilirejelea mashambulizi siku ya Jumanne

Vikosi vya serikali vilirejea mashambulizi siku ya Jumanne

Maafisa wa Afya katika mji wa Alleppo nchini Syria wamelazimika kusitisha huduma za hospitali katika eneo la mashariki linaloshikiliwa na waasi kufuatia siku kadhaa za mashambulizi makali ya mabomu.

Mkurugenzi wa huduma za matibabu mashariki mwa Aleppo Abdul Baset Ibrahim, amelaumu mashambulizi ya saa arubaini na nane ya ndege za kivita za Urusi na Syria dhidi ya maeneo yanayokaribiana na mahospitali.

Maeneo yanayokaribiana na hospitali yalishambuliwa
Maeneo yanayokaribiana na hospitali yalishambuliwa

Hapo jana kulikuwa na ripoti kuwa hospitali ya watoto imelengwa huku kukiwa na hofu kwamba shabulio hilo lilikuwa ya gesi ya chlorine.

Mshauri wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Jan Egeland, amesema wakaaazi wa Aleppo wanakabiliwa na hali ngumu.

Mapema wiki hii Urusi imekanusha kufanya oparesheni katika maeneo hayo.

Maandamano ya kumpinga Rais yaendelea Korea Kusini

Maandamano yafanyika kwa wiki ya nne mfululizo Korea Kusini

Maandamano yafanyika kwa wiki ya nne mfululizo Korea Kusini

Kwa wiki ya nne mfululizo maelfu ya watu wanaendelea kuandamana katika mji mkuu wa Seoul, nchini Korea Kusini, ili kumshinikiza Rais Park Guen Hye ajiuzulu.

Rais huyo amekataa kuitikia wito wao na kusalia madarakani.

Rais Park Guen Hye
Rais Park Guen Hye

Hapo jana lijitokeza hadharani wa mara ya kwanza, zaidi ya wiki moja, kama ishara ya kuonyesha nia yake ya kutaka kuendelea kuhudumu kama rais.

Waandamanaji hao wameghadhabishwa na hatua yake ya kumruhusu mwanamke anayedaiwa kuwa rafiki yake wa karibu, Choi Soon-sil, kutumia ushawishi wake kufanya ulaghai.

Choi Soon-sil
Choi Soon-sil

Mwanamke huyo kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa usalama.

Thursday, 17 November 2016

Mwanamume mwenye HIV aliyefanya mapenzi na wanawake 104 Malawi

Eric Aniva alikiri kufanya mapenzi na wanawake pamoja na wasichana 104

V 2
Eric Aniva alikiri kufanya mapenzi na wanawake pamoja na wasichana 104

Uamuzi wa kesi ya mwanamme mmoja nchini Malawi unatarajiwa kutolewa wiki hii, baada ya kuiambia BBC kuwa alifanya mapenzi na wasichana kama sehemu ya mila.

Eric Aniva alikamatwa mwezi Julai kufuatia amri ya rais, baada ya kukiri kuwa alifanya mapenzi yasiyo na kinga na wasichana walio na umri wa hadi miaka 12, na kuwa kimya juu ya hali yake ya kuugua ugonjwa wa ukimwi.

Aniva anasema kuwa alipewa vibarua na familia za wasichana hao kushiriki mapenzi nao, kwa tamaduni ambayo jamii inaamini kuwa huwezesha wasicha kuingia utu uzima.

"Tunaamini kuwa ikiwa mjane au mwanamme aliyefiwa hawezi kusafishwa kwa njia ya mapenzi, huenda kisa kibaya kikafuatia kama kifo kwa majane au mwanamme aliyefiwa au kwa ukoo mzima," alisema mhudumu mmja wa jamii.

Malawi
Malawi

Wakati rais wa Malawi Peter Mutharia aliamrisha mwanamme huyo akamatwe, alitaka Aniva ashtakiwe kwa kuwabaka wasichana wadodgo, lakini hata hivyo hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.

Kwa hivyo sasa Aniva ameshtakiwa kwa kushiriki utamaduni wenye kuumiza, chini ya kipengee cha chato cha sheria ya usawa wa kijinsia nchini Malawi ambapo alifanya mapenzi na wajane.

Katika kesi hii wanawake wawili wamejitokeza ili kutoa ushahidi dhdi ya Aniva, licha ya mmoja kusema kuwa alifanya mapenzi naye kabla ya mila hiyo kupigwa marufuku huku mwingine naye akisema kuwa alifanikiwa kukimbia kabla ya kitendo cha ngono kufanyika.

Hadi miaka michache iliyopita, mila hii ilikuwa maarufu katika wilaya yote kwa mjane kufanya mapenzi na mwanamme mara tatu kwa siku kwa usiku tatu au nne.

Eric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti
Eric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti

Mwanamme huyo anaweza kuwa ndugu wa mmewe, lakini wakati mwingine mtu kutoka nje hutafutwa kama Aniva kuweza kushiriki kitendo hicho.

Ikiwa aliyefiwa ni mwanamme, mwanamke hutafutwa kuweza kufanya mapenzi naye.

Kinachowatisha watu nchini Malawi kuhusu Aniva, ambaye alidai kufanya mapenzi na wanawake 104 pamoja na wasicha, wakati wa mahojiano na BBC ni kuwa hukuachana na tabia hiyo licha ya kugundua kuwa alikuwa na virusi vya HIV

"HIV inaua. Itakuwaje mtu mwenye virusi kufanya kile alichokifanya? Nafikiri yeye ni shetani. Ningekuwa hakimu ningempa hukumu ya kifo na kifungo cha maisha," alisema mhubiri Paul Mzimu.

clouds stream