Thursday, 9 February 2017

Mkuu Wa Wilaya Shinyanga Afuata Nyayo Za Makonda Anasa Watu


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na Waanndishi wa Habari ofisini kwake.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na Waanndishi wa Habari ofisini kwake leo.
img-20161130-wa0008

Sakata la Madawa ya Kulevya limeanza kutikisa kwa kasi mkoani Shinyanga ambapo watu 17 wamekamatwa wakituhumiwa kutumia madawa ya Kulevya pamoja na Mirungi.

Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati anazungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo amesema ofisi yake imepokea majina ya watu 20 wanaojihusisha na masuala ya madawa ya kulevya.

Amesema hadi sasa watu 17 wanashikiliwa na Polisi, ikiwa ni kutii agizo la Rais Dkt. John Magufuli aliyetaka Vita dhidi ya Dawa za Kulevya ienee nchi nzima.

Amesema baada ya kupata majina kutoka kwa wananchi kuwa watu hao wanajihusisha na masuala ya madawa ya kulevya sasa kimeundwa kikosi kazi cha kufuatilia ukweli kuhusu watu hao.

Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwa watumiaji na wauzaji wa madawa ya kulevya hawapo Dar pekee wapo nchi nzima hivyo wanaendelea na msako kila kona ya mtaa ili kuhakikisha kuwa madawa ya kulevya yanakomeshwa mkoani humo.

Mkalimani Feki Aliyepotosha Maneno Ya Mtalii Atiwa Mbaroni


muongozzzzzzzzzzzimg-20161130-wa0008

Jeshi la Polisi limemtia mbaroni Muongoza watalii (Tour Guide) anayeonekana katika kipande cha picha ya video akipotosha tafsiri ya matamshi ya Mtalii aliyekuwa amemaliza kutembelea Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA).

Katika video hiyo ambayo imesambaa sana katika mitandao ya kijamii hasa WhatsApp, inamuonesha mtalii huyo ambaye jina lake halijafahamika maramoja akisema katika lugha ya kigeni (kingereza)kuwa safari yake nchini Tanzania imekuwa nzuri na kufurahia safari yake huku akikutana na watanzania waliokuwa na ukarimu na upendo kwake.

Muongozaji huyo anaonekana akitafsiri maneno ya mtalii huyo na kupotosha na kuanza kusema vitu ambavyo havikusemwa na mtalii huyo kama anawashangaa watanzania wakilalamika njaa wakati wana maua, hivyo wapike maua wale na kumtaja Rais

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa ameagiza kukamatwa kwa mkalimani huyo feki mara tu baada ya kuona video hiyo.

“Tayari nilitoa maagizo mtu huyo atafutwe na akamatwe mara moja na kwa taarifa nilizopewa leo ni kuwa mtu huyo ameshakamatwa kwenye lango la geti la Nabi Serengeti na yupo rumande huko Mugumu,” amesema. 

UPDATE: Manji Azuiwa Asiondoke,Arudishwa Kituo Cha Polisi Gwajima Akiwasili Kituoni


Manji akizuiwa na askari polisi kutoka nje ya kituo cha polisi.
Manji akizuiwa na askari polisi kutoka nje ya kituo cha polisi.
img-20161130-wa0008

Kutoka Central Police Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Yanga na Mfanyabiashara, Yusuph Manji amezuiwa kutoka kituoni hapo baada ya kufanyika mahojiano.

Polisi wameagizwa wamzuie asiondoke na amerudishwa kituoni hapo huku ikidaiwa kuwa ni kwa ajili ya kumsubiri Kamanda Simon Sirro.

Wakati huohuo, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anadaiwa kuwasili kituoni hapo kuonana na Kamanda Simon Sirro.

Mchungaji Gwajima amewasili kituo cha polisi majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake, kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya, aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake.

clouds stream