Tuesday, 31 October 2017

Nape Akana Taarifa Iliyozagaa Mitandaoni



Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.

Baada ya Mbunge Lazaro Nyalandu kujiuzulu na kuhamia chama cha Chadema,Nape amekana taarifa iliyoenea mitandaoni kuwaatazungumza na  Waandishi wa Habari leo.

Kupitia ukurasa wake wa Mitandao ya kijamii Nape amesema hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema
kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

“Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina ‘press conference’
kesho” aliandika Nape Nnauye.

Zitto Kabwe Akamatwa Na Polisi Dar


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe.


Hatimaye, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam na amepelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Hayo yameibanishwa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis ambapo amesema sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaamkatika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini.

Hivi karibuni Zitto kabwe amekua akikosoa serikali kuhusiana na hali ya uchumi wa nchi kukua suala ambalo Zitto amesema
haliendani na uhalisia wa maisha ya wananchi

Kenyatta atangazwa mshindi wa urais Kenya akiwa na kura 7.5m

 Uhuru KenyattaRaisi Uhuru Kenyata

Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.

Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita.

Hiyo ni asilimia 38.84.

Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.

Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe.

"Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu," amesema.

Bw Odinga alikuwa ametarajiwa kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw Chebukati.

Taarifa zinasema ameamua kufanya hivyo hapo kesho.

Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati

MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee7,483,89598.28
Raila Odinga (Alisusia)ODM73,2280.96
Mohamed Abduba DidaARK14,1070.19
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea8,2610.11
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea6,0070.08
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea5,5540.07
John Ekuru AukotThirdway Alliance21,3330.28
Cyrus JirongoUDP3,8320.05

Bw Chebukati amesema anaamini uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Mwenyekiti huyo amesema mambo aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki yalitimizwa.

Amesema walitaka kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.

"Hata tulibadilisha tarehe kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.

Kadhalika, amesema alikuwa na kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.

"Naweza kusema kwa uhakika, kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake kikatiba," amesema.

"Na haki hii mtu anafaa kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."

Bw Chebukati anasema alishangaa kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.

Hata hivyo, anasema ndani ya tume nao walimwogopa.

"Hatutaweza kufurahisa kila mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria niliyojitolea kuilinda," amesema.

Matokeo yalivyokuwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu

MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee8,203,29054.27
Raila OdingaODM6,762,22444.74
Mohamed Abduba DidaARK38,0930.25
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea16,4820.08
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea13,2570.09
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea42,2590.28
John Ekuru AukotThirdway Alliance27,3110.18
Cyrus JirongoUDP11,7050.08

clouds stream