Afisa huyo anayehudumu katika afisi ya gavana iliyoko kusini mwa Kivu alisema kuwa watu watatu waliaga dunia, akiwemo mlinzi aliyeshindwa kuwakabili wafungwa hao walipokuwa wakitoroka.
Polisi wameshika doria Bukavu,jiji ambalo limejengwa kandokando ya ufuo wa ziwa Kivu mashariki mwa Kongo ili kuwasaka.
Mkazi mmoja ameiambia BBC kwamba watu waliojawa na hofu walikuwa wakijificha katika nyumba zao.
Mwanahabari wa BBC Maud Jullien, anasema kuwa kutoroka gerezani imekuwa jambo la kawaida nchini humo – wafungwa wapatao 240 walitoroka katika mji mwingine wa Mashariki ya taifa hilo chini ya mwaka mmoja uliopita.
Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la AFP kwamba walinzi wa magereza walishindwa kukabiliana n awafungwa hao ambao ‘’walichukua silaha na kuharibu milango ya magereza.”
Wakazi wanasema milio ya risasi ilisikika asubuhi hiyo jijini.
Wanaharakati wa vyama vya raiya wanasema kuwa huenda idadi ya waliotoroka ikawa zaidi, kwani idadi jumla ya wafungwa waliokuwemo gerezani ni 1,500 huku maafisa husika wakikisia kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wafungwa walikuwa wametoroka.
Magereza nchini Kongo mara nyingi huwa na idadi kubwa kupita kiasi na hali ya maisha huwa mbovu kwa wafungwa.