Mshambulizi wa Uruguay, Luis Suarez aliungata mkono unaomlisha alipofunga mabao mawili na kuisaidia Uruguay kasajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uingereza katika mchuano wao wa kundi D, huko Sao Paulo. Matokeo hayo yameiwacha Uingereza mguu nje mguu ndani ya kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.
Hata ingawa mkufunzi wa Uingereza Roy Hodgson hakubadilisha kikosi chake kutokana na kile kilichocheza dhidi ya Italia huko Manaus katika mechi yao ya awali, alimpa Wayne Rooney nafasi ya kucheza katikati, nyuma ya mshambulizi Daniel Sturridge.
Kufwatia kichapo cha 3-1 dhidi ya Costa Rica, Oscar Tabarez alifanya mabadiliko 5 katika kikosi kilichochuana na Uingereza.
Suarez aliyekua na jeraha la goti pia alijumuishwa katika kikosi hicho.
Suarez aliupiga mpira wa kona ambao ulimpata Hart akiwa hayuko tayari, hata hivyo aliweza kuutoa mpira huo nje na kusababisha kona nyingine.
Nafasi nzuri ya Uingereza ya kupata bao, ilikuja pale Sturridge alipoupiga mpira ambao uligusa mkono wake Diego Godin naye refa wa mechihiyo Carlos Velasco akawapa waingereza mpira wa adhabu katikati ya ya uwanja.
Nafasi nzuri ya Uingereza ya kupata bao, ilikuja pale Sturridge alipoupiga mpira ambao uligusa mkono wake Diego Godin naye refa wa mechihiyo Carlos Velasco akawapa waingereza mpira wa adhabu katikati ya ya uwanja.
Rooney aliupiga lakini ukatoka nje, hata ingawa hatua chache tu.
Timu zote mbili zilipata nafasi nzuri na umiliki , bila kukamilisha mashambulizi .
Hata hivyo Rooney alikaribia kufunga bao lake la kwanza katika michuano yote ya kombe la dunia ambayo ameshiriki katika dakika ya 31.
Shuti yake Steven Gerrard iliingia katika eneo la penalti la Uruguay naye Rooney na Godin wakapigania mpira huo ambao Rooney aliupata kwa kichwa ila tu uligonga mwamba wa lango la Uruguay .
Nicolas Lodeiro aliupata mpira katikati ya uwanja na akampisha Edinson Cavani.
Mchezaji huyo wa Paris Saint Germain alimpiga chenga Phil Jagielka na akampata Suarez aliyefunga kwa kichwa.
Hayo, katika dakika ya 39, Suarez akawapa La Celeste, bao la kwanza.
Kama walivyofanya dhidi ya Italia, Uingereza pia ilishambulia muda mfupi baadaye. Rooney alimpa Sturridge pasi naye akawapita walinzi wa Uruguay na kutoa mkwaju uliookolewa na , kipa wa Uruguay Fernando Musclera.
Hata hivyo waingereza walikataa kufa moyo.
Dakika kumi na tano kabla mchuano kukamilika, Rooney alipata mpira kutoka kwa Glen Johnson naye akafunga bao la kusawazisha.
Bao lake la kwanza katika michuano yoyote ya kombe la dunia.
Timu zote mbili zilianza kutafuta bao la ushindi.
Mpira wake Musclera ulimfikia Suarez na mchezaji huyo wa Liverpool akaupita ulinzi wa Uingereza na kufunga bao la pili dhidi ya Hart zikiwa zimesalia dakika tano mechi kukamillika.
Uingereza bado ina matumaini ya kuendelea iwapo wataishinda timu ya Costa Rica na kusubiri ikiwa matokeo ya mechi baina ya Italia na Uruguay yatakuwa mazuri kwao.
Uingereza sasa watafurushwa kutoka kwenye kombe la dunia Brazil 2014 iwapo wapinzani wao katika kundi hilo Costa Rica watatoka sare ama kushinda Italia katika mechi yao ya pili itakayochezwa Ijumaa.