Friday 20 June 2014

IVORY COAST KUPOTEZA MECHI DHIDI YA COLOMBIA


Gevinho alifungia Ivory Coast bao la kufutia machozi
Colombia ilipiga hatua kubwa ya kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia baada ya kuilaza Ivory Coast mabao 2-1 katika mechi yao kali ya kundi C, iliyochezwa katika uga wa Estadio Nacional, Brasilia.
James Rodriguez aliiweka Colombia kifua mbele baada ya saa moja kupitia kichwa, naye mchezaji wa akiba Juan Quintero akongeza la pili.

Hata hivyo hawakuweza kusawazisha.Bao lake Gervinho liliwapa Ivory Coast matumaini.
Timu zote mbili zilikua zimeshinda mechi zao za kwanza za ya kombe la dunia.
Mfungaji bao la Colombia Rodriguez
Mkufunzi wa Colombia, Jose Pekerman alitumia kikosi kile kile alichokitumia katika mechi ya kwanza walipoishinda Ugiriki mabao 3-0.
Ivory Coast, tena walimwacha nje Didier Drogba akiuguza jeraha la paja, hata ingawa alicheza mchezo mzuri walipowashinda Japan 2-1 katika mechi yao ya kwanza huko Recife.
Ivory Coast sasa wanahitaji kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Ugiriki ilikuwa na matumaini ya kumaliza katika nafasi ya pili ya kundi hilo na kusonga mbele katika hatua ya maondoano.
Colombia inaongoza kundi hilo ikiwa na jumla ya alama 6 huku Ivory Coast ikiwa ya pili na alama 3 kufuatia ushindi wao wa kwanza dhidi ya Japan.
Teofilo Gutierrez ndiye aliyetangulia kushambulia katika eneo la penalti la The Elephants wa Ivory Coast.
Mlinzi wa The Elephants, Didier Zokora alizuia shambulizi la Juan Cuadrado baadaye.
Kibofu kilitupwa uwanjani na mashabiki wa Colombia
Serge Aurier, mlinzi wa Ivory Coast anayehusishwa na uhamiaji kwa timu ya Arsenal, alipiga shuti kutoka yadi 18 nao ukaokolewa kwa urahisi na kipa wa Colombia, David Ospina.
Katika kipindi cha pili, refa muingereza, Howard Webb, alikataa wito wa penalti kwa timu ya Ivory Coast baada ya Gervinho kuangushwa na Mario Yepes, nahodha wa Colombia.
Katika dakika ya 55, Zokora alionyeshwa kadi ya manjano baada ya kumkosea Cuadrado hivyo basi hataucheza mchuano wa mwisho wa makundi dhidi ya Ugiriki.
Colombia ilichukua uongozi katika dakika ya 64 baada ya mshambulizi wa Monaco, Rodriguez kufunga bao kwa kichwa baada ya kona.
Mashabiki wa Colombia
Muda mfupi baada ya hapo, The elephants walifanya mabadiliko mengine.
Salomon Kalou aliingia katika nafasi ya Max Gradel.Hata hivyo, Colombia walifunga bao la pili katika dakika ya 70.
Gutierrez alimpa Juan Quintero pasi wawili hao walipoishambulia safu ya ulinzi ya Ivory Coast.
Quintero aliuchukua mpira nje ya eneo la penalti na kuupiga kwenye wavu wa The Elephants.
Dakika tatu baadaye, Gervinho alifunga bao lao la kufutia machozi, ambalo pia ni bao lake la pili katika michuano hii.
Ivory Coast sasa wanahitaji ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Ugiriki ikiwa wana matumaini ya kuendelea mbele katika michuano hii ya kombe la dunia.

clouds stream