Ghana yaanza kupaa Kimataifa, yazindua gari lake
Nchi ya Ghana imefungua njia kwa nchi nyingine barani Afrika kufuatia kuanza utengenezaji wa magari aina ya Kantanka ambayo ni pamoja na lile aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo. Babaake ni m’bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini. Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kwa mujibu wa mmoaja wa raia nchini humo amesema watu wanapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni imara.