Madiwani 20, Wenyeviti 6 kwa Lowassa, watua Chadema
Madiwani 20 wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Monduli, wamejiunga na Chadema kufuatia Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa jina lake kukatwa wakati akiomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama hicho.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara kiongozi wa Madiwani hao, Julius Kalanga kutoka Kata ya Lepurko ambaye pia alikabidhi kadi yake na za wenzake 19 wa CCM kwa viongozi wa Chadema huku wakisisitiza kuwa wamefanya uamuzi mgumu ambao Lowassa amekuwa akiusema mara kwa mara katika safari yake ya siasa.
Madiwani waliohama kutoka chama cha Mapinduzi kwenda Chadema
Madiwani waliohama chama ni Kalanga mwenyewe, Edward Lenanu, Bazir Siamini, Sigur Olekibinti, Loti Yamat, Goodluck Lerunya, Pashet Sengurumi, Yase Runja, Gidion Kimongishu, Dora Kipuyo, Mary Morindat, Sara Lomayan na Halima Lusinde.
Kata ya Engaruka, Engutoto, Esilalei, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mferejini, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini.
Dotto Mlacha, Hawa Nyambiry, Alex Kamanda, Sion Kapela, Maria Lemta, Onesmo Naikoyo, Shaban Adam, Enditosidai Naikulo na Elifuraha Simon.
Wengine ni Dinna Solomon, Loti Naparana, Jocy Laizer, Edward Mathayo, Piniel Loning’o, Napir Mukare, Inot Leringa, Kalaine Lowassa, Maria Mepukori, Mary Stivin na Edward Kone.
Katika hatua nyingine, tangia kukatwa jina lake Mbunge huyo hajazungumza jambo lolote ambapo alitaka kuzungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam hata hivyo mkutano huo uli ahirishwa kwa madai kwamba amechelewa kuwasili jijini Dar es salaam akitokea mkoani Dodoma.