Hotel ya Kendwa Rocks yateketea kwa moto visiwani Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole mwakilishi
wa Hotel ya Kendwa iliyoteketea kwa moto Zanzibar.
Kwa mujibu wa wahudumu wa Hotel hivyo wameiambia Hivisasa Blog kwamba moto huo ulizuka na kuenea kwa kasi kutokana na upepo mkali majira ya saa nne asubuhi jana ambapo hasara ya takribani bilioni moja inasadikiwa kupatikana kutokana na moto huo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ametembelea katika eneo la tukio kujione hali ilivyo. Mara baada ya kutembelea amewapa pole wamiliki wa hotel hiyo kufuatia hasara kubwa waliyopata.