Argentina yafanya mauaji yaipiga Paraguay 6-1,Di Maria apiga mbili Copa America

Winga Timu ya Taifa ya Argentina na Klabu ya Manchester United ya Wingereza,Angel di Maria.
Timu ya Taifa ya Argentina imetinga kwa kishindo hatua ya fainali ya Copa America baada yakuitandika Paraguay kipigo cha mbwa mwizi cha magoi 6-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa
usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Marcos Rojo (15), Javier Pastore (27), Angel Di Maria (47, 53),
Sergio Aguero (80) na Gonzalo Higuain (83), huku goli la kufutia machozi kwa Paraguay likifungwa
na Lucas Barrios (43).