Uhaba wa mafuta nchini wachukua sura mpya Bungeni
Serikali imesema kwamba akiba ya Mafuta ya Petrol nchini Tanzania inatoshelea hadi siku 40.Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa madai kutokea uhaba wa mafuta siku kadhaa zijazo.
Akijibu hoja ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyeomba Bunge hilo kujadili hoja hiyo kwa njia ya dharula kwa kuwa linamaslahi kwa uchumi wa taifa Naibu wazii wa Nishati na Madini Charles Mwijage amesema mafuta yapo na kuna meli zipo nje maji marefu zinakuja nchini zikiwa na shehena ya mafuta.
Amewahakikishia wananchi kuwa nchi haiwezi kuapata tatizo la uhaba wa mafuta huku akisisitiza kuwa kwa kushirikiana na TCRA wanawatafuta waliosambaza taarifa hizo.
Naye Naibu waziri wa Fedha Adam Malima amesema serikali itahakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya mafuta kama kwaida.