Urais 2015: Lowassa afunga mahesabu ya Wadhamini Morogoro

Katibu
wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge, akionyesha fomu zenye
orodha ya majina ya wanachama wa ccm,104,03 waliomdhamini kugombea
urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa CCM na
wananchi wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa akitoa shukrani katika
kuhitimisha Mkoa wa mwisho wa kupokea orodha ya majina ya wadhamini.
Akiwa Mkoani Morogoro Lowassa amepata wanaccm 104,038 waliojitokeza kumdhamini katika safari yake ya matumaini aliyoa ianza mara baada ya kutangaza nia ya kugombea urais uwanja wa sheikh Abeid Karume jijini Arusha may 29 maka huu.
Lowassa pamoja na watia nia wengine CCM wanatakiwa kurejesha fomu za urais makao ya Makuu ya CCM mkoani Dodoma wiki hii huku mwisho wa kurejesha fomu hizo ikiwa ni julai 3,2015.
Baada ya kurejesha fomu watasubiri matokeo ya mchujo utaofanywa na kamatia Kuu CCM itakayoketi na kuanza zoezi a uchujaji.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na chama hicho inaonesha kuwa vikao vya uchujaji vitakuwa kama ifuatvyo,
Kamati ya usalama na Maadili Zanzibar 4/7/2015
Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya Taifa 5/7/2015
Kamati ya Usalama na Maadili Taifa 8/7/ 2015
Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa 9/7/2015
Halmashauri kuu ya Taifa 10/7/2015
Mkutano mkuu wa Taifa 11-12/7/2015