Thursday 14 January 2016

CCM Waibua Mbinu Mpya Kuimaliza Ukawa 2016

CCM Waibua Mbinu Mpya Kuimaliza Ukawa 2016

Tarehe January 13, 2016
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kipo katika mpango kabambe wa kujiimarisha mara ya kupata misuko suko katika uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba  25,2015 ambapo Wanachama wake walijiondoa na hivyo kuleta mpasuko ndani ya chama hicho.
Miongoni mwa wanasiasa walio jitoa katika chama hicho  hali iliyopelekea kuondoka na wanachama wa CCM ni aiyekuwa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa,Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na kada mkongwe ndani ya chama hicho Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Makada hao walileta mtikisiko ndani ya chama cha Mapinduzi huku watafiti wa masuala ya kisiasa wakishidwa kubashiri nani angeibuka mshindi katika kiti cha Urais  ambapo licha ya mchuano mkali  Mgombea wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli aliibuka kidedea na kumshinda Edward  Lowassa kwa asilimia 58.46 huku lowassa akiambulia  asilimia  39.97.
Baada ya kutangazwa mshindi  wa Urais Dkt. John Pombe Magufuli alianza kazi kwa kasi kubwa na kuahid kutumbua majipu yaliyokwamisha mipango mbalimbali ya serikali kutokana na upotevu wa mapato katika sekta za umma ikwemo Bandarini na Mamlaka ya Mapato pamoja na kuwaondoa watendaji wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma na kuundoa mfumo wa kufanya kazi kwa mazoea.
Ikiwa ni miezi 2 imepita tangu Magufuli aanze kazi, kasi yake imeonesha kuwamaliza nguvu wapinzani ambao mara kwa mara wamekuwa wakidai kwamba kiongozi huyo wa CCM anatekeleza sera zao huku baadhi ya wananchi wakihoji sera za upinzani kwa sasa baada ya ile ya ufisadi kuwa haina mashiko tena mbele ya jamii.
Mwaka huu wa 2016 ifikapo  februari 05 Chama hicho  kitakuwa kinatimiza miaka 39 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977.
Hivyo Chama hicho kinatarajia kufanya maadhimisho ya aina yake pamoja na kuja na mipango kabambe  ya kujiimarisha ili kuvipunguza  nguvu vyama vya Upinzani  ikiwemo Chadema na CUF.
Kwa mujibu wa taarifa yake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na uenezi Nape Moses Nnauye (Mb) amesema kwamba sherehe hizo kwa mwaka huu zitakuwa za aina yake kufuatia kuweka malengo katika Ujenzi wa Chama kwa kuzoa wanachama wapya katika maeneo mbalimbali nchini.
Ujenzi huo wa chama utahusisha, Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama, kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi, kushiriki na kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na  kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
Shughuli nyingine ni  kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji, kufanya usafi wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii.
Kaulimbiu ya sherehe hizo ni Sasa Kazi, Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.
Aidha,Uzinduzi wa maadhimisho ya kumbukumbu ya hiyo utafanyika tarehe 31 Januari, 2016 Unguja, Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.
Kwa upande wa  Kilele cha maadhimisho hayo  kitakuwa ni  Februari 06, 2016 mjini Singida ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.

clouds stream