Sunday, 19 March 2017

Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi'

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa "kihistoria"
img-20161130-wa0008

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.

Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.

Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.

Tangazo hilo linatokea wakati wa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, anapofanya mazungumzo na viongozi wa China huko, Beijing.

Awali, Bwana Tillerson, aliionya Marekani kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kwamba inaweza kuharibu mambo hata zaidi.

clouds stream