Thursday, 16 March 2017

Mahakama yazuia marufuku mpya ya Trump Marekani

Waandamanaji karibu na White House Machi 11

Maandamano yamefanyika Marekani kupinga marufuku hiyo
img-20161130-wa0008

Mahakama moja katika jimbo la Hawaii imezuia utekelezaji wa marufuku mpya ya usafiri iliyokuwa imetangazwa na Rais Donald Trump.

Marufuku hiyo ilizuiwa saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa saa sita usiku Alhamisi.

Jaji Derrick Watson alisema ushahidi uliotolewa na serikali katika kutetea marufuku hiyo ni wa kutiliwa shaka.

Serikali ilikuwa imejitetea mahakamani ikisema marufuku hiyo inalenga kuimarisha usalama wa taifa.

Rais Trump ameeleza uamuzi huo wa jaji kuwa wa kushangaza na akasema mahakama imevuka mpaka.

Agizo lililokuwa limetolewa na Trump, ambalo lilifaa kuanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ungepiga marufuku kwa miezi mitatu raia kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi kuzuru Marekani.

Mataifa hayo ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen.

Aidha, ingezuia wakimbizi kuingia Marekani kwa kipindi cha siku 120.

Bw Trump amesisitiza kwamba hatua hiyo inalenga kuzuia magaidi wasiingie Marekani lakini wanaoipinga wamesema inabagua makundi ya watu.

Marufuku nyingine ya awali aliyokuwa ameitoa Januari ilisababisha mtafaruku na maandamano kabla ya kuzuiwa na jaji mjini Seattle.

Akihutubu katika mkutano wa hadhara mjini Nashville, Tennessee Jumatano jioni, Bw Trump alisema uamuzi huo wa jaji mjini Hawaiii uliifanya Marekani "kuonekana dhaifu".

Alisema ataendelea na kesi hiyo "hadi itakapofikia", ikiwemo kwenda Mahakama ya Juu.

ALiongeza: "Tutashinda."

President Donald Trump holds a rally at the Municipal Auditorium in Nashville, Tennessee, March 15, 2017Hawaii ni mojawapo ya majimbo kadha ya Marekani yanayopinga marufuku hiyo.

Mawakili wa jimbo hilo waliambia mahakama kwamba marufuku hiyo inakiuka katiba ya Marekani kwamba watu hawafai kubaguliwa kwa misingi ya asili yao.

Jimbo hilo pia limesema marufuku hiyo itaathiri utalii na uwezo wa serikali ya jimbo hilo kupokea wanafunzi na wafanyakazi kutoka mataifa ya nje.

clouds stream