Saturday 4 March 2017

Uhispania Yateua Waziri Wa ‘Ngono’, Kazi Yake Kubwa Hii Hapa

Bunge la Uhispania.
Bunge la Uhispania.
img-20161130-wa0008

Serikali ya Uhispania imeamua kuteua Waziri wa Masuala ya Ngono ikiwa ni katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa Afisa Mkuu wa masuala ya ngono.

Hatua ya kubuni wizara nzima ya inayojihusisha na ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa ya kupungua kwa idadi ya watu. 

Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilimali zilizopo huko Uhispania hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua tena kwa kasi ya kutisha.

Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Naye Waziri wa Elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa Serikali na Baraza la Mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.

Kazi kubwa ya Waziri huyo mpya ni kuja na mbinu na mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania.


clouds stream