Thursday, 8 June 2017

WANAUME WENYE VIPARA WAGEUZWA ‘DILI’ MSUMBIJI


bald_black_guy

IMG-20170426-WA0006

Polisi nchini Msumbiji wameonya kuwa wanaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi, pamoja na matambiko fulani, baada ya kuuliwa kwa wanaume wawili kama hao mwezi uliopita.

Wanaume hao wawili wenye upara na ambapo mmoja wao alipatikana akiwa amekatwa kichwa na viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, waliuliwa katika Mkoa wa Zambezi.

“Mwezi uliopita, mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa kwa washukiwa wawili,” msemaji wa polisi Inacio Dina alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Maputo.

Kwa mujibu wa BBC Mjini Maputo, baadhi ya watu wana imani potofu kuwa watu wenye vipara wako na dhahabu kwenye vichwa vyao.

Visa vya kuuliwa watu wenye upara kwa maswala ya uchawi havijaripotiwa siku za nyuma. Washukiwa ni vijana wa Msumbiji, waliowaambia polisi kuwa viungo hivyo vingetumiwa kwa uchawi na matambiko nchini Tanzania na Malawi.

Tanzania inafahamika duniani kwa watu wenye matatizo ya ngozi kuuwawa na viungo vyao kutumika kwenye matambiko ya kichawi.

clouds stream