Wednesday, 21 June 2017

JPM: Waombeeni Wauaji Wa Pwani Waokoke


Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania wote kuwaombea wahalifu wanaofanya mauaji huko Mkoani Pwani, ili waweze kuokoka na kujua thamani ya damu ya mtu.

Rais Magufuli amesema hayo mapema jana wakati akihutubia mkutano wake wa kwanza katika ziara ya siku tatu Mkoani humo.

“Niwaombe wananchi wa Pwani, msishirikiane na watu waovu kwakuwa wanachelewesha sana maendeleo na ndio maana huko Kibiti hakuna hata kiwanda na hakuna imani ya dini yoyote ile inayosema watu wauane,” amesema.

Hatahivyo, amesema kuwa wauaji hao wameshaanza kuuona moto na kuonya kuwa Serikali ya Awamu ya Tano sio ya kuchezea.

“Watanyooka tu, wameshaanza kunyooka, kama wapo hapa wanaotusikiliza basi wakapeleke salamu.Niwaombe sana, tuwaombee hawa watu waokoke, ili wajue damu ya mtu ina thamani kubwa sana,” ameongeza.

clouds stream