Thursday, 8 June 2017

UTAFITI: BODABODA , BAISKELI JANGA JIPYA KWA NGUVU ZA KIUME

Madereva bodaboda wakerwa mwenzao kutelekezwa baada ya kupigwa risasi.

IMG-20170426-WA0006

Kazi ya kuendesha baiskeli za kubeba abiria pamoja na baiskeli zinazopatikana kwenye vituo vya mazoezi (gym) vimebainika kuwa chanzo cha kupunguza uwezo wa wanaume wanaposhiriki tendo la ndoa.

Hayo yamebainika kupitia utafiti uliofanywa hivi karibuni na jopo la wataalam wa afya ya uzazi likiongozwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, Wamalwa nchini Kenya.

Matokeo ya utafiti huo uliowahusisha waendesha baiskeli (bodaboda) 115 wenye umri kati ya miaka 18 na 40, katika eneo la Bungoma, Mashariki mwa Kenya, ulibaini kuwa asilimia 35.9 walikuwa na matatizo ya uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa ipasavyo, kwakuwa wameathiriwa misuli ya uume.

Vijana hao walipimwa na wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wakishirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, ambapo majibu yalionesha kuwa asilimia 39.5 walikuwa na tatizo la kusisimua misuli ya uume.

Utafiti huo ulionesha kuwa vijana hao waliathirika kutokana na kutumia nguvu nyingi katika kuendesha baiskeli na kwamba walioendesha baiskeli kwa muda wa saa 60 au zaidi kwa wiki ndio waliathirika zaidi.

Wamalwa alitahadharisha pia kuwa vijana wengi walio kwenye vituo vya kufanyia mazoezi (gym) wakiendesha baiskeli zisizokuwa na vizuizi maalum dhidi ya sehemu za uume, wako kwenye hatari ya kukutwa na tatizo la kutokuwa na uwezo wa kushiriki ipasavyo tendo la ndoa.

Aidha, matokeo ya utafiti huo pia yanaendana na matoekeo ya tafiti zilizofanywa na watafiti wengine sita wa Chuo Kikuu cha Moi zilizowahusisha vijana 131 wa mjini Eldoret, wenye umri kati ya miaka 18 na 56. Kati ya waliopimwa, asilimia 76 walibainika kuwa na matatizo ya kutosisimua ipasavyo misuli ya uume.

“Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani,” Mhadhiri Wamalwa ameviambia vyombo vya habari.

clouds stream