Tuesday, 6 May 2014

HOTEL BATHROOMS (MUONEKANO MZURI KWA MABAFU NA VYOO VYA HOTELI)

Kama una mpango wa kujenga au kuboresha hoteli yako basi kuna sehemu ambayo kila mtu lazma atizame akiwa anatafuta hoteli ya kulala, sehemu hio ni chooni na bafuni. Wengi wanapenda kuwa na eneo la bafu ambalo linavutia na ambalo halita mtia shaka na usafi wa hoteli au pia uimara wa eneo lako.
Kwa asilimia kubwa, uzuri wa eneo hili nyeti unaeza hata kuchangia katika pesa ambayo mtu anaweza kulipia kwa chumba.
Kwa ushahuri, ukitaka bafu la hoteli liwe zuri unaweza fanya yafuatayo:

  • Jitahidi kupata tiles ambazo zinaleta muonekano wa usafi zaidi. Ogopa brown.
  • Jitahidi kufananisha rangi ya vitu vya ziada kama mataulo na vinginevyo na rangi ya tiles zako.
  • weka mataulo eneo lililo rahisi kuchukua ndani ya bafu na sio kitandani. 
  • Cheza na rangi za taa kuleta mvuto wa kipekee.
Hizi hapa ni baadhi ya picha za muundo mzuri wa bafu na choo kwa hoteli. 




















Friday, 2 May 2014

MATATIZO YA KULIPA KODI. MASTAA WALIOTESEKA KISA KODI HOLLYWOOD.

1. Martha Stewart
Mwana mama huyu ambae ni bingwa wa kupamba nyumba na kutengeneza bustani za mastaa wa hollywood kabla ya kutiwa ndani alipata kesi ya kukwepa kodi kiasi cha $220,000 ambapo ni kodi na faini zilizomkabili.

2. Wesley Snipes

Mmarekani mweusi huyu ambae ni maarufu sana kutokana na filamu yake ya blade amekua kivutio kikubwa kwa wasaka kodi hasa baada ya kuingiza fedha nyingi na kukwepa kodi kwa ya kama $17 millioni. Jamaa alipigwa jela miaka mitatu baada ya hayo kubainika.

 3. Nicolas Cage

Muigizaji maarufu nicholas cage alibainika kukwepa kodi kiasi cha $6 million ambapo hio imesemekana ni pesa alizoingiza katika miaka aliyotoa filamu zake kama national treasure na leaving las vegas.    Kutokana na hayo, jamaa aliweza kuweka mambo sawa na kulipia kodi hio.

4. Marc Anthony

Mwanamziki huyu inasemekana aliweka malimbikizo ya kiasi cha sillingi $2.5 millioni ambayo ni sehemu a kodi iliyokwepwa pamoja na faini alizotozwa.

5. Lauryn Hill: 

Mwanadada huyu alipigwa jela miezi mitatu baada ya kubainika kukwepa kodi ya kiasi cha shilingi $ 1 million. Lauryn kashotoka kwa sasa na kabanwa mwaka mzima kwa shows mbalimbali.




Thursday, 1 May 2014

GARI LANGU LIKO WAPI? GOOGLE INAJUA.


Google imetoa application mpya ambayo inaweza kusaidia kujua wapi umepaki gari lako au gari lako liko wapi katika muda flani unayoitaji kujua kua iko wapi.
Mfumo huu wa kugundua gari lako liko wapi inatumika kwa simu za android na utakua unatumia GPS kujua eneo husika ambapo gari lako lipo kwa kuweka kumbukumbu kwenye simu yako. Japokua kuna changamoto sababu ya mwendo kasi wa gari na kasi ya internet lakini appilication hii imeanza kupata umaarufu na kuvutia zaidi watumizi wa android smartphones.

clouds stream