Monday, 5 January 2015

BOKO HARAM WATEKA WAVULANA WENGINE 40

BOKO HARAM WATEKA WAVULANA WENGINE 40


Takriban wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wakazi walio  kitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku moja tu kabla ya mwaka mpya.
Watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho  wakiwa   katika gari aina ya pick up na kuwaagiza wanaume wote kutoka nje ili kuweza kusikiliza mahubiri ndipo waliwakamata na kuwateka vijana hao ambao walipelekwa  katika msitu jirani wa Sambisa.
Mwaka uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 kutoka shule moja ya bweni kazkazini mwa Nigeria.

PALESTINA KUJIUNGA ICC, ISRAEL YAJIPANGA KUSITISHA MISAADA

PALESTINA KUJIUNGA ICC, ISRAEL YAJIPANGA KUSITISHA MISAADA


.
Maafisa nchini Israel wanasema kuwa serikali hiyo itasimamisha fedha kwenda kwa utawala wa Palestina siku moja baada ya utawala huo kutuma ombi la kutaka kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.
Maafisa ambao hawakutajwa walisema kuwa baraza la mawaziri nchini Israeli limeamua kuzuia kutolewa kwa dola milioni 125 ambazo hutumiwa kuendesha shughuli za serikali ya utawala wa Palestina.
Hatahivyo afisa kutoka utawala huo (Saeeb Erekat) ameitaja hatua hiyo ya Israeli kama adhabu iliyo kinyume na sheria.
Ikiwa utawala wa Palestina utafanikiwa kujiunga na mahakama ya ICC itasababisha Israeli kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kutokana na uhalifu kwenye sehemu inazokalia.

Sunday, 4 January 2015

MSICHANA WA MIAKA 7 ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE



MSICHANA WA MIAKA 7 ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE



Ndege iliyopata ajali.
Ndege iliyopata ajali.
Mtoto mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja katika jimbo la Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege aliyopanda.
Kwa mujibu wa jeshi la  polisi ndege hiyo baadaye ilionekana  imeanguka huku watu wanne wakiwa wamefariki katika kaunti ya Lyon yapata kilomita 50 mashariki mwa mji wa Paducah
Kituo cha runinga cha NBC nchini Marekani kimesema kuwa msichana huyo alimwarifu mtu aliyemfungulia mlango kwamba wazazi wake wote  walifariki katika ajali hiyo ya ndege.

clouds stream