PALESTINA KUJIUNGA ICC, ISRAEL YAJIPANGA KUSITISHA MISAADA
Maafisa nchini Israel wanasema kuwa
serikali hiyo itasimamisha fedha kwenda kwa utawala wa Palestina siku
moja baada ya utawala huo kutuma ombi la kutaka kuwa mwanachama wa
mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.
Maafisa ambao hawakutajwa walisema kuwa baraza la mawaziri nchini
Israeli limeamua kuzuia kutolewa kwa dola milioni 125 ambazo hutumiwa
kuendesha shughuli za serikali ya utawala wa Palestina.Hatahivyo afisa kutoka utawala huo (Saeeb Erekat) ameitaja hatua hiyo ya Israeli kama adhabu iliyo kinyume na sheria.
Ikiwa utawala wa Palestina utafanikiwa kujiunga na mahakama ya ICC itasababisha Israeli kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kutokana na uhalifu kwenye sehemu inazokalia.