Sunday, 1 February 2015

Arsenal yafanya mauaji

Arsenal yafanya mauaji


Winga wa Arsenal Theo Walcot akishangilia goli lake
Winga wa Arsenal Theo Walcot akishangilia goli lake
Arsenal yaanza vyema mwezi February baada ya kuibugiza Aston Villa goli 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates jioni ya leo.
Olivier Giroud alifunga bao la kwanza dakika ya nane akimalizia kazi nzuri ya Mesut Ozil, baadae Ozil alifunga goli ambalo lilikatalia na mwamuzi lakini akafunga linguine dakika ya 56.
Theo Walkot aliye rejea akitokea kwenye majeruhi ya muda mrefunae akafunga bao la tatu dakika ya 64, Sant Cazorla la nne dakika ya 75 na Hector Bellerin akamaliza la tano dakika ya 90 ya mchezo huo.

Ivory Coast yatinga nusu fainali

Ivory Coast yatinga nusu fainali



Wilfred Bony (kulia) akishangilia goli na wachezaji wenzake wa Ivory Coast
Wilfred Bony (kulia) akishangilia goli na wachezaji wenzake wa Ivory Coast
Ivory Cost imeitupa nje ya mashindano timu ya Ageria kwa kuifunga goli 2-1katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Jumapili usiku kwenye uwanja wa Estadio de Malabo.
Ivory Coast ndio waliokua wa kwanza kupata bao la kuongoza mfungaji akiwa ni nyota mpya wa Manchester City Wilfred Bony dakika ya 26. Baada ya mapumziko Algeria walijipanga vizuri na kusawazisha goli hilo dakika ya 51 kupitia kwa Hilal Soudan aliyefunga kwa kichwa.
Dakika ya 68 ya mchezo Bony akaifungia Ivory Coast goli la pili baada yakuunganisha kwa kichwa mpira waadhabu ndogo uliopigwa na Yaya Toure, lakini Gervinho akashindilia msumari wa moto kwa vigogo hao alipofunga goli la tatu katika dakika ya 90+4 kuihakikishia timu yake ushindi.
Hatua ya nusu fainali itazikutanisha Ghana dhidi ya wenyeji Equatorial Guinea, wakati Ivory Coast watamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ndanda FC yaikwamisha yanga taifa

Ndanda FC yaikwamisha yanga taifa


Kikosis cha timu ya Dar es Salaam Young Africans 'Yanga'
Kikosis cha timu ya Dar es Salaam Young Africans ‘Yanga’
Dakika 90 zimemalizika za mechi kati ya Yanga dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara huku kukiwa hakuna mbabe wa pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Washambuliaji wa Yanga bado wameonekana kukosa umakini kwani wameendelea kukosa magoli mengi ya wazi kutokana na nafasi nyingi walizo zitengeneza. Dakika ya 51 msahmbuliaji raia wa Liberia Sherman alikosa goli akiwa ndani ya eneo la hatari, baada ya shuti lake kugonga mwamba na kutoka nje. Lakini dakika ya 77 Mrwanda alishindwa kuifungia timu yake baada ya kukosa goli akiwa yeye na kipa.
Kocha wa Yanga Van der Pluijm alifanya mabadiliko na kuwaingiza washambuliaji wake wote, akimtoa Sherman na nafasi yake kuchukuliwa na Tambwe na baadae akamtoa Ngasa na kumuingiza Tegete. Lakini mbinu zake hazikuzaa matunda.
Kipa wa Yanga Ally Mustapha ‘Bathez’ alifanya kazi ya ziada dakika ya 78 kuokoa mara mbili mashuti ya kustukiza ya washambuliaji wa Ndanda FC.
Ernest Mwalupani alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na mwamuzi wa mchezo huo Martin Saanya baada ya awali kupewa kadi ya njano.

clouds stream