Tuesday, 24 June 2014

NITAJUTA- MKUBWA NA WANAWE

UHOLANZI KUKUTANA NA MEXICO


Uholanzi kuvaana na Mexico mkondo wa pili
Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Mabao ya Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na Memphis Depay yaliyowapa ushindi dhidi ya Chile katika mechi ngumu iliyochezewa jijini Sao Paulo.
Mechi hiyo ilikosa msisimko na kuishia sufuri bin suifuri kufikia muda wa mapumziko ,Lakini Fer alifunga kwa kichwa katika dakika ya 77, kabla ya Depay kufunga katika dakika ya mwisho.Timu zote mbili zilikuwa tayari zimefuzu kwa raundi ya pili baada ya kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya Uhispania na Australia.
Huenda Chile wakachuana na Brazil katika mechi za muondoano, huku upande wa Luiz Van Gaal ukitarajia kuchuana na aidha Mexico au Croatia.
Uholanzi ilikuwa bila mshambulizi Robin Van Persie ambaye alikuwa anatumikia marufuku baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Uholanzi kuvaana na Chile mkondo wa pili
Chile nayo ilimpumzisha kiungo cha kati Arturo Vidal ambaye kukosekana kwake kuliadhiri mchezo, kwani ilichukua muda kabla ya walinda lango kuugusa mpira.
Mshambulizi wa Barcelona Alexis Sanchez alionekana kutaka kufunga bao la kwanza kwa Chile kwa weledi wake na pasi ambazo ziliwahangaisha mabeki wa Uholanzi kwa muda.
Arjen Robben alikuwa karibu kuendeleza rekodi yake ya kufunga bao katika kila mechi baada ya mkwaju wake kukosa lango.
Ilikuwa hadi dakika ya 65 wakati mlindalango Jasper Cillessen alipolazimika kuokoa mkwaju wa Sanchez uliopigiwa karibu na lango.
Hilo liliwatia waholanzi motisha na kumfanya Robben kupiga mkwaju uliomlenga Claudio Bravo katika lango la Chile baada ya kuwapiga chenga mabeki kabla ya Depay kuokoa kutoka kwa mlindalango kwa kuondoa katika maeneo ya hatari.
Kufutia ushindi huo Uholanzi wanatuchana na mshindi wa pili katika kundi A yaani Mexico.
Huku Chile ikiratbiwa kuvaana na mshindi wa kundi A yaani Brazil katika mechi za maondoano .

MAUJI ZAIDI YAWAKUTA WAKENYA


Mashambulizi ya Mepeketoni yalisababisha vifo vya watu 60
Takriban watu watano wameuawa katika shambulizi lengine katika eneo la pwani ya Kenya.
Mauaji hayo yametokea karibu na eneo ambako mashambulizi mengine yalifanyika wiki jana na kusababisha vifo vya watu zaidi ya sitini.
Maafisa wanasema kuwa kundi la watu waliokuwa wamejihami walivamia kijiji cha Witu ambacho kiko umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Mpeketoni.
Hakuna aliyedai kufanya mashambulizi hayo hadi kufikia sasa.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi ya wiki jana katika mji wa Mpeketoni karibu na Lamu.
Rais Uhuru Kenyatta, hata hivyo aliwalaumu wanasiasa kwa mauaji hayo.
Mkuu wa jimbo la Lamu, Stephen Ikua, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo usiku wa kuamkia leo.
Al-Shabab, lilisema kuwa mashambulizi ya hapo awali yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa kuwepo wanjeshi wa Kenya nchini Somalia.
Ndege za kivita za Kenya zilifanya mashambulizi mengine dhidi ya kambi za wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua wapiganaji 80 mwishoni mwa wiki.

clouds stream