Tuesday, 26 May 2015

COMMERCIAL SPACE FOR RENT ( GdB HOUSE ), TEGETA.


Real Madrid wafukuza kocha

Real Madrid wafukuza kocha

Tarehe May 26, 2015
_83218614_carlo_ancelotti_getty-2

Baada ya kushindwa kuifikisha Real Madrid kwenye hatua ya fainali kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya na pia kushindwa kuchukua ligi kuu nchini Hispania imekuwa kama moja ya mambo yaliyofanya kocha wa Carlo Ancelotti kufukuzwa. Carlo Ancelotti alipofanya mahojiano na waandishi wa habari siku ya ijumaa alisema anaamini ataendelea kuifundisha timu hiyo msimu ujao huku wachezaji kama Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakiamini kuwa na kocha wao msimu ujao.
Maamuzi ya Real Madrid kumfukuza Carlo Ancelotti yalifanyika jana baada ya rais wa timu hiyo Florentino Perez kuonyesha wazi siku za karibuni kwa maneno yake kuwa kocha huyo amebakiza siku chache kwenye klau hiyo, nuamuzi huo wa Real Madrid unaongeza tetesi kwenye masikio ya mashabiki wa Real Madrid kuwa kocha atakaechukua kiti hicho ni Rafa Benitez.

Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10

Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10

Tarehe May 26, 2015
Rais Jakaya Kikwete atua mkuu wa wilaya mpya.
Rais Jakaya Kikwete atua mkuu wa wilaya mpya.
Rais Jakaya Kikwete  amemteua Bw.  Antony Peter mavunde kuwa mkuu wa wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imebainisha kwamba  licha ya kumteua mkuu wa wilaya mpya mmoja   pia   awahamisha wakuu wa wilaya wengine 10 kwa lengo la kuongeza ufanisi katika wilaya mbalimbali nchini.
Katika mabadiliko hayo,Rais kikwete amemhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka  wilaya ya Mkalama mkoni Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya  mpya ya  Kyerwa mkoani Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni kanali benedict Kulikela kitenga ambaye alifariki dunia aprili 20 mwaka huu.
Wengine ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka wilaya ya Dodoma kwenda  wilaya ya  Mvomero mkoa wa  Morogoro. Dkt Jasmine Tisike kutoka wilaya ya Mpwapwa  kwenda  Dodoma. Agnes Elias Hokololo kutoka wilaya  ya Namtumbo  mkoani Ruvuma kwenda wilaya ya Tunduru, Fadhili Nkurlu kutoka wilaya ya Misenyi mkoani kagera kwenda  wilaya ya mkalama.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa  Chande Bakari Nalicho amehamishwa  kutoka wilaya ya  Tunduru kwenda Wilaya  ya  Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka wilaya ya  Mvomero kwenda Misenyi , Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Karagwe mkoani Kagera kwenda  wilaya ya biharamulo mkoani humo humo.
Elias Choro John Tarimo  amehamishwa  kutoka  wilaya ya Biharamulo kwenda wilaya ya  Chunya  mkoani  mbeya   pamoja  na Deodatus   Lukasi Kinwiro kutoka wilaya ya Chunya kwenda wilaya ya  Karagwe mkoani Kagera.

clouds stream