Dkt.Kikwete amteua mkuu mpya wa Wilaya na kuwahamisha wengine 10
Rais Jakaya Kikwete amemteua Bw. Antony Peter mavunde kuwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imebainisha kwamba licha ya kumteua mkuu wa wilaya mpya mmoja pia awahamisha wakuu wa wilaya wengine 10 kwa lengo la kuongeza ufanisi katika wilaya mbalimbali nchini.
Katika mabadiliko hayo,Rais kikwete amemhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka wilaya ya Mkalama mkoni Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni kanali benedict Kulikela kitenga ambaye alifariki dunia aprili 20 mwaka huu.
Wengine ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka wilaya ya Dodoma kwenda wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro. Dkt Jasmine Tisike kutoka wilaya ya Mpwapwa kwenda Dodoma. Agnes Elias Hokololo kutoka wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwenda wilaya ya Tunduru, Fadhili Nkurlu kutoka wilaya ya Misenyi mkoani kagera kwenda wilaya ya mkalama.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Chande Bakari Nalicho amehamishwa kutoka wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi , Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Karagwe mkoani Kagera kwenda wilaya ya biharamulo mkoani humo humo.
Elias Choro John Tarimo amehamishwa kutoka wilaya ya Biharamulo kwenda wilaya ya Chunya mkoani mbeya pamoja na Deodatus Lukasi Kinwiro kutoka wilaya ya Chunya kwenda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.