Matusi’ yawachefua wananchi kampeni za Makongoro
Tarehe
September 28, 2015
Mbunge wa Afrika Maashariki Makongoro Nyerere.
Wananchi mkoani Dodoma wamesikitishwa na kampeni za chama cha
Mapinduzi kupitia mjumbe wa timu ya kampeni ambaye ni Mbunge wa Afrika
Mashariki Makongoro Nyerere.
Hayo yamebainishwa na wananchi mkoani Dodoma mara baada ya kufanyika
mkutano wa kampeni za CCM ambapo Makongoro Nyerere aliweka sera za CCM
kando na kuanza kutoa kashfa kwa wagombea wa vyama vya siasa hususani
Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa na mgombea Ubunge Benson
Kigaila.
Moja ya kauli zake katika mkutano huo ni kudai kuwa Ikulu hakuna
makabuli hivyo Lowassa anaumwa na kuna uwezekano akafia Ikulu, Mbali na
hilo alisema Ikulu siyo wodi ya wagonjwa na sehemu ya makaburi hivyo ni
vyema mtu anayetakiwa kwenda Ikulu ni mtu mwenye nguvu.
Aliongeza kwa kuwashangaa watu wa UKAWA kuwa wana roho ngumu sana kutembea na mtu ambaye amechoka vile.
Baadhi ya wakazi mkoani humo walionesha kusikiktishwa na kauli hizo
wakidai kwamba walikwenda katika mkutano huo kusikiliza sera na jinsi
chama hicho kitakavyotatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi
ikiwemo uhaba wa maji.
Pasipo kutaka majina yao yaandikwe mtandaoni wananchi hao wamesema
inashangaza Makongoro kutumia muda mwingi kumchafua mgombea mwingine kwa
kuwa wananchi wao ndio watakao chagua pumba na mchele,hivyo wamedai ni
vema kada huyo akaheshimu afya ya mtu mwingine kwa kuwa ni mipango ya
mungu.
Mwananchi mwingine alidai CCM ya hivisasa sio sawa na ile anayoijua
kwa sababu imekuwa na kampeni za ‘matusi’ ambapo licha ya matusi hayo
hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi suala
linalo onesha kuwa huenda tume hiyo imeegemea upande mmoja wa chama
tawala.