Tuesday, 19 July 2016

Moyes Alamba Dili Lingine


Tarehe July 19, 2016Aliyekuwa Kocha wa Manchester United David Moyes.
Aliyekuwa Kocha wa Manchester United David Moyes.
Aliyekuwa Kocha wa Manchester United David Moyes.
Kocha wa zamani wa Everton na Manchester United, David Moyes amepata dili la kuwafundisha makocha nchini Jordan,Moyes ambaye aliwahi kuinoa Real Sociedad ya Hispania amekuwa akiwanoa makocha hao wa nchini Jordan ili kuwaongezea ujuzi.
Pamoja na makocha wengine lakini zaidi Moyes amekuwa akiwanoa makocha wa timu za taifa za Jordan.

Ibrahimovic Amtolea Uvivu Cantona


Tarehe July 19, 2016Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan Ibrahimovic.
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amejibu vijembe kutoka kwa gwiji wa Klabu hiyo Eric Cantona baada ya gwiji huyo kusema kuwa kuna mfalme mmoja tu katika klabu hiyo na siku zote atabaki kuwa yeye.
Siku chache baada ya Ibrahimovic kujiunga na klabu ya Man United akitokea Paris Saint German (PSG), Cantona aliandika katika mitandao ya kijamii ujumbe ufuatao:
“Just one last thing, there can only be one King in Manchester. You can be the Prince if you want to. And the No 7 is yours if you are interested. That is my welcome gift to you… The King is gone! Long live the Prince.”
Baada ya kauli hiyo, Ibrahimovic ameliambia gazeti la Aftonbladet, “I admire Cantona and I heard what he said.”
“But I won’t be King of Manchester. I will be God of Manchester,” ameongeza.
Wachezaji hao wote wawili wanajulikana kuwa na sifa ya utukutu huku Cantona aliondoka United akiwa hana maelewano mazuri na aliyekuwa kocha wake Ferguson na Ibrahimovic naye aliwahi kukwaruzana na Pep Guadiola wakati wapo Barcelona lakini pia aliwahi kufungiwa kwa kosa la kumpiga muamuzi.

BAVICHA Nao Bado ‘Ngunguri’


Tarehe July 19, 2016Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Wakati maandalizi ya Mkutano Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakipamba moto, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limesema lengo lao la kufanya kikao chao cha Kamati ya Utendaji Mjini Dodoma bado lipo palepale licha ya Jeshi la Polisi kusema kikao hicho hakitafanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema hivi karibuni kuwa kikao cha Bavicha hakitofanyika kwa sababu itakuwa ni mwendelezo wa vurugu zao.
Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita  amesema  baraza hilo lipo kwenye hatua ya mwisho ya maandalizi ya kikao hicho kitakachohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka Mikoani.
Amesema wajumbe hao wataanza kuwasili leo Mjini Dodoma na kwamba hawana wasiwasi na kikao hicho kwa sababu ni cha ndani  na sio mkutano wa hadhara ambao umepigwa marufuku na polisi.
Mwita amesema kikao hicho kitakuwa cha siku mbili kuanzia Julai 20 hadi 21 na kwamba, kitahudhuriwa na Mameya na Wenyeviti Vijana wa Halmshauri zinazoongozwa na Chadema.
Kuhusu kauli ya Kamanda Mambosasa, Mwita amesema polisi ilishatoa maelekezo ya kuruhusu vikao vya ndani.
“Taarifa ya Mambosasa hatujaishangaa kwa sababu ni desturi yake kujichanganya, leo anasema hivi kesho vile. Tunamtaka atulie asubiri tumpe taarifa ni wapi kikao chetu kitanyika kwa njia ya amani,” amesema Mwita

clouds stream