Tuesday, 19 July 2016

BAVICHA Nao Bado ‘Ngunguri’


Tarehe July 19, 2016Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Baadhi ya wajumbe wa BAVICHA
Wakati maandalizi ya Mkutano Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakipamba moto, Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) limesema lengo lao la kufanya kikao chao cha Kamati ya Utendaji Mjini Dodoma bado lipo palepale licha ya Jeshi la Polisi kusema kikao hicho hakitafanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema hivi karibuni kuwa kikao cha Bavicha hakitofanyika kwa sababu itakuwa ni mwendelezo wa vurugu zao.
Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita  amesema  baraza hilo lipo kwenye hatua ya mwisho ya maandalizi ya kikao hicho kitakachohudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka Mikoani.
Amesema wajumbe hao wataanza kuwasili leo Mjini Dodoma na kwamba hawana wasiwasi na kikao hicho kwa sababu ni cha ndani  na sio mkutano wa hadhara ambao umepigwa marufuku na polisi.
Mwita amesema kikao hicho kitakuwa cha siku mbili kuanzia Julai 20 hadi 21 na kwamba, kitahudhuriwa na Mameya na Wenyeviti Vijana wa Halmshauri zinazoongozwa na Chadema.
Kuhusu kauli ya Kamanda Mambosasa, Mwita amesema polisi ilishatoa maelekezo ya kuruhusu vikao vya ndani.
“Taarifa ya Mambosasa hatujaishangaa kwa sababu ni desturi yake kujichanganya, leo anasema hivi kesho vile. Tunamtaka atulie asubiri tumpe taarifa ni wapi kikao chetu kitanyika kwa njia ya amani,” amesema Mwita

clouds stream