Tuesday, 6 June 2017

Cheick Tiote: Mchezaji wa zamani wa Newcastle afariki dunia

Cheick Tiote

Cheick Tiote alichezea Newcastle mechi 156 mashindano yote.
IMG-20170426-WA0006

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa an miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China, msemaji wa mchezaji huyo amesema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikaa miaka saba Newcastle na kuwachezea mechi 138 ligini.

Alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari.

"Ni kwa huzuni kubwa ambapo ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi," msemaji wake alisema.

"Hatuwezi kusema zaidi kwa sasa na tunaomba kwamba familia yake iheshimiwe kipindi hiki kigumu. Tunaomba maombi yenu."

Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Misri, Saudi Arabia na Bahrain kufunga anga zake kwa ndege za Qatar

qatar

shirika la ndege la Qatar
IMG-20170426-WA0006

Misri inafunga anga zake kwa ndege za Qatar katika mzozo wa kidiplomasia unaozidi kukua huku Saudi Arabia na Bahrain nazo zikitarajiwa kuchukua hatua kama hiyo leo Jumanne.

Nchi kadha zimekata uhusiano na Qatar, baada ya kuishutumu kwa kuunga mkono ugaidi katika eneo la Ghuba.

Raia wa Qatar nchini Bahrain, Saudi Arabia na Muungano wa Milki ya nchi za kiarabu wamepewa muda wa wiki mbili kuondoka.

Qatar inakana kunga mkono wanamgambo na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni ametaka kuwepo mazungumzo.

Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo hautaathiri chochote katika utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharula tangu mzozo huo ulipoibuka siku ya Jumatatu wiki hii.

Sunday, 28 May 2017

Simba SC Bingwa Kombe La ASFC

Wachezaji na viongozi wa Simba SC wakifurahia taji a Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania Bara (ASFC) msimu wa 2016/17
IMG-20170426-WA0006
Wachezaji na viongozi wa Simba SC wakifurahia taji a Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania Bara (ASFC) msimu wa 2016/17.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (ASFC), Nahodha wa klabu ya Simba SC Jonas Mkude baada ya kuitandika Mbao FC kwa mabao 2-1 baada ya muda wa nyongeza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (ASFC), Nahodha wa klabu ya Simba SC Jonas Mkude baada ya kuitandika Mbao FC kwa mabao 2-­1 baada ya muda wa nyongeza.
Nahodha wa Simba SC Jonas Mkude akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 ikiwa ni zawadi ya bingwa wa ASFC
Nahodha wa Simba SC Jonas Mkude akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 ikiwa ni zawadi ya bingwa wa ASFC.
Mkwaju wa penalti wa Shiza Kichuya katika muda wa nyongeza ulioipa taji kabla yake mbele ya Mbao FC kwa mabao 2-1.
Mkwaju wa penalti wa Shiza Kichuya katika muda wa nyongeza ulioipa taji kabla yake mbele ya Mbao FC kwa mabao 2-­1.
Shiza Kichuya akiiunuliwa juu baada ya ushindi huo.
Shiza Kichuya akiinuliwa juu baada ya ushindi .
Shabiki wa Simba akiwa na msumeno bandia ulioandikwa maneno ya kuisuta Mbao FC
Shabiki wa Simba akiwa na msumeno bandia ulioandikwa maneno ya kuisuta Mbao FC.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuatilia fainali hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akifuatilia mpambano huo.
Mshambuliaji wa Ivory oast Fredrick Blagnon aliyetokea benchi na kuipa Simba SC bao la kuongoza akishangilia.
Mshambuliaji wa Ivory oast Fredrick Blagnon aliyetokea benchi na kuipa Simba SC bao la kuongoza akishangilia.
Wafungaji wa mabao wa Simba SCBlagnon na Kichuya wakipongezana baada ya kazi nzito.
Wafungaji wa mabao wa Simba SCBlagnon na Kichuya wakipongezana baada ya kazi nzito.
Fainali za ASFC msimu wa 2016/17 upande wa mashabiki
Upande wa mashabiki.
Manyika
Mlinda mlango chaguo la tatu la Simba SC Peter Manyika Jr akiwafariji wachezaji wa Mbao FC baada ya kumalizika kwa fainali.

clouds stream